RC MAKALLA AWAHAKIKISHIA WAKAZI WA KIPANDE CHA FELA KUJA MWANZA MJINI MALIPO YAO YA FIDIA KUPISHA MRADI WA SGR YAMEKAMILIKA
*Asema malipo yao yapo hatua za mwisho kulipwa
*Ofisi yake imejipanga kukabiliana na aina yoyote ya hujuma kwenye mradi
*Ampongeza Mkandarasi kwa kasi nzuri.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA Amos Makalla amewahakikishia wakazi wa kipande cha kutoka Fela kuja Mwanza mjini cha kilomita 20 wanaotakiwa kupisha mradi wa Treni iendayo kasi SGR utaratibu wa malipo yao ya fidia upo katika hatua za mwisho kulipwa.
Akizungumza na uongozi wa mradi huo kwenye ukumbi mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa lengo la kufanya tathmini ya mradi huo,Mhe.Makala amewataka wananchi hao kuondoa shaka kwani mchakato wa malipo yao sasa upo Hazina.
"Hatua zote za msingi kuhusiana na fidia kwa wakazi wa maeneo hayo umefanyika,na wakati wowote kuanzia sasa malipo yatafanyika naomba niwahakikishie,"amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.
Ameongeza kuwa Ofisi yake imejipanga kikamilifu kukabiliana na aina yoyote ya hujuma itakayofanyika kwenye mradi huo kwani kwa matendo hayo yatachangia kuzorotesha na kuchelewesha kukamilika kwa mradi huo.
"Nichukue nafasi hii kumpongeza sana Rais wetu Dkt.Samia Suluhu kwa kuhakikisha mradi huu unaendelea na fedha kutolewa kwa wakati",CPA Makalla
"Tupo katika hatua nzuri kukamilisha mradi huu,kipande cha Isaka-Mwanza chenye kilomita 341 kinajengwa kwa ubia wa Kampuni ya CCECC na CRCC zote kutoka China,"Christopher Kalisti,Meneja Mradi SGR LOT 5.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.