RC MAKALLA AWAOMBA WADAU WA ELIMU KUJITOKEZA KUING'ARISHA MWANZA KUCHANGIA MFUKO WA MAENDELEO YA ELIMU DUNIANI
*Asema faida ya kuchangia mfuko huo ni Tanzania kuzidi kuimarika kwenye Sekta ya elimu
*Aonesha matumaini wadau kumuunga mkono kwa wingi kwenye mkutano wa kitaifa mwezi ujao
Wadau wa elimu Mkoani Mwanza wameombwa kujitokeza kwa wingi kuunga mkono mpango wa uchangiaji elimu kupitia mfuko wa maendeleo ya elimu Duniani GPE ili Tanzania iweze kunufaika na msaada wa Dolla milioni 50 endapo nchi hii itaonesha utayari huo.
Akizungumza leo kwenye kikao kifupi cha kuelimishana kuhusu mpango huo kilichofanyika kwenye ukumbi mkubwa wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA.Amos Makalla amesema faida ya kupata fedha hizo ni kubwa katika kuzidi kujiimarisha kwenye sekta ya elimu hapa nchini
"Ndugu zangu wadau wa elimu tunaona jitihada za Serikali ya awamu ya sita inazofanya kwenye sekta hii ya elimu,hivyo tukifanikiwa kuzipata fedha hizo zitakwenda kujikita katika kuboresha miundombinu,na kuwajengea zaidi uwezo walimu wetu,"CPA Amos Makalla
Aidha ameonesha Imani kwa wadau hao kumuunga mkono kwa wingi katika uchangiaji huo ili katika kikao cha kitaifa kitakachofanyika Agosti 25,2023 kitakacho wajumuisha wakuu wa mikoa wote Mkoa wa Mwanza ushike nafasi za juu katika kuunga mkono mpango huo.
"Tanzania ni mnufaika wa Mfuko huu tangu mwaka 2013 na ufadhili wa kwanza tulipata dola milioni 94.8 na zilisaidia mpango wa KKK yaani kusoma,kuandika na kuhesabu na Mkoa wa Mwanza umepata Shs bilioni 2.8 kuimarisha mkakati huo",amefafanua Dkt.Nicholous Gati,Afisa ufuatiliaji na tathmini,Mfuko wa maendeleo ya elimu Duniani,GPE.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.