RC MAKALLA AWAPONGEZA TIC KUHAMASISHA WATANZANIA KUWEKEZA NCHINI
*Abainisha kuwa Miradi ya Kimkakati kuinua Uchumi wa Nchi*
*Awataka watanzania kuwekeza nchini kwa maendeleo ya Taifa*
*Awapongeza kwa kuweka mazingira rafiki zaidi ya upatikanaji wa leseni*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla amekipongeza Kituo cha Uwekezaji nchini kwa kuhamasisha watanzania kujivunia uwekezaji nchini ili kukuza uchumi wao na kuweka mazingiza rafiki kwao kujihusisha.
Akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho aliyeambatana na timu ya wafanyakazi leo januari 08, 2024 Ofisini kwake Mhe. Makalla amesema uamuzi wa kutoa Elimu kwa wafanyabiashara na makundi mengine juu ya uwejezaji ili kutoa hamasa waweze kuwekeza zaidi nchini.
Makalla amesema siku za nyuma watanzania walikua na kasumba kwamba uwekezaji ni kwa wananachi wa nje ya nchi pekee lakini kutokana na juhudi za Kituo hicho hivi sasa wameanza kuelewa kwamba ni suala la Wote hata wazawa.
Amesema kuwa Mkoa wa Mwanza umekua ukiongoza kwenye kutoa pato la Taifa kwa kushika nafasi ya pili ukiongozwa na Mkoa wa Dar Es Salaam na kwamba kwa shabaha ya Mkoa kwa sasa ni kuongeza juhudi kwenye uwekezaji kupitia sekta za uvuvi, kilimo, mifugo na uchukuzi.
Halikadharika, Mhe. Makalla amewapongeza kituo hicho kwa kuweka mazingira rafiki zaidi ya upatikanaji wa leseni na kusaidia wananchi wengi zaidi kuamua kujihusisha na shughuli za uchumi za kuwekeza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini Gilead Teri amesema taasisi hiyo inafanya Uhamasishaji ili Watanzania waweze kujikita kwenye kuwekeza mitaji yao nchini badala ya kupeleka nje ili waweze kukuza nchi yao.
Ndugu Teri amesema wameona Viwanda vingi sana Mkoani Mwanza na kwamba vitasaidia kukuza uchumi kwani Sekta za Uvuvi, kilimo, uchukuzi kupitia miradi ya kimkakati inayojengwa na Madini vimeimarishwa sana siku za karibuni.
Ameongeza kuwa pamoja na ubora wa sheria ya Uwekezaji ya 2023, mifumo ya TEHAMA inasaidia zaidi kuweka urahisi wa kuhusisha watanzania wengi zaidi kwenye uwekezaji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.