RC MAKALLA AWATAKA NSSF KUHARAKISHA KUIDHINISHA MABORESHO ILI MKANDARASI WA UJENZI HOTELI AKAMILISHE HARAKA
*Asema Mwanza ni mji wa kimkakati kitalii lazima wachangamkie fursa*
*Awataka kukamilisha taratibu za manunuzi ili mkandarasi aende kasi*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla amewataka Mfuko wa Jamii (NSSF) kuharakisha taratibu za manunuzi ili mkandarasi anayejenga Hoteli ya kisasa ya kitalii ya nyota tano jijini Mwanza aendelee na ujenzi na kukamilisha kwa wakati.
Mkuu wa Mkoa ametoa maagizo hayo leo Januari 10, 2024 alipofika kukagua ujenzi wa Hoteli hiyo na kubaini kuwa ujenzi umesimama jambo ambalo litakwamisha ukamilishaji mwezi Julai mwaka huu kama ambavyo walibainisha siku za nyuma.
"Sasa nyie NSSF inaonesha mapendekezo yameshatolewa lakini msipofanya maamuzi mtachelewa zaidi ya hapa msilete visingizio vya bodi kukutana kumpa muda mkandarasi na kuidhinisha vitu fulani hapo tutachelewa zaidi nataka mkandarasi apewe kazi afanye." Makalla.
Aidha, amewataka NSSF kukamilisha taratibu za ukandarasi wa ujenzi wa Hoteli hiyo kufuatia kuongezwa kwa muda wa mkataba kufikia Disemba 2024 badala ya Mwezi Julai 2024 kama walivyoahidi siku za nyuma.
"Hoteli hii ni Muhimu sana kwa ukanda huu, Mwanza ni mji wa kimkakati nanyi mmepata nafasi ya kumiliki hoteli ya kisasa halafu mnaichezea wakati pale uwanja wa ndege linajengwa jengo la abiria na sehemu ya manunuzi (Shopping Mall), changamkeni." CPA makalla.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.