RC MAKALLA AWATAKA WAJASIRIAMALI KUTUMIA SEMINA NA VIFAA MTAJI KUTOKA AMO FOUNDATION KUKUZA BIASHARA ZAO
*Awataka kuwa na vipaumbele kwenye kusimamia biashara moja kwa umakini*
*Aipongeza AMO Foundation kwa kuweka huduma ya upimaji Afya*
*Atoa wito kwa vikundi kurejesha mikopo ili kuleta ufanisi wa mradi*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla amewataka wajasiriamali kutumia semina na vifaa mtaji kutoka AMO foundation kutumia semina ya mafunzo na Vifaa mtaji watakavyokopeshwa kujiimarisha kiuchumi.
CPA Makalla ametoa wito huo leo Machi 06, 2024 wakati akikagua maendeleo ya Kongamano la siku nne la uwezeshaji kwa Wajasiriamali lililoandaliwa na Taasisi hiyo kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mkoani Mwanza.
Makalla amesema katika kuhakikisha wanafanikiwa kukuza mitaji yao ni lazima wawe na nidhamu ya matumizi ya fedha na kurejesha mikopo kwa wakati ili pia vikundi vingine viweze kufikiwa kwenye uwezeshaji.
Aidha, ametumia wasaa huo kushukuru taasisi hiyo kwa kutoa huduma za upimaji afya kwenye magonjwa mbalimbali bila malipo yanayokwenda sambamba na kongamano hilo kwa wajasiriamali pamoja na wananchi.
Bi. Amina Good, Mkurugenzi wa Shirika la AMO foundation amebainisha kuwa shirika hilo limeamua kushirikiana na Serikali katika kutoa huduma za kijamii na ukuzaji wa mitaji kwa wajasiriamali kwa kuwapatia vifaa mitaji.
"AMO foundation tumeamua kushirikiana na Serikali kutoa huduma kwa jamii na katika kuwapata wanufaika wa vifaa hivi kama Pikipiki, mitungi ya gesi na majiko tumeshirikiana na Halmashauri kuwapata wajasiriamali kuanzia ngazi za vitongoji hadi Mkoa." Bi. Amina.
Kongamano hilo lenye Kaulimbiu isemayo; 'Uwajibikaji wetu ndio uhai wa Uchumi wetu' limewakusanya wajasiriamali kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mwanza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.