• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

WADAU WA KILIMO WATAKIWA KUWEKA MBINU MADHUBUTI KUONGEZA UZALISHAJI

Posted on: February 10th, 2026

Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Mwanza anaesimamia Uchumi na Uzalishaji Bi. Candidah Kyamani leo Februari 10, 2026 amefungua mafunzo maalumu yaliyowakutanisha wauzaji na wakaguzi wa pembejeo za kilimo, mifugo na uvuvi kutoka Halmashauri za Mkoa huo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Nyakahoja.

Akifungua mafunzo hayo Bi. Kyamani amewasihi wadau hao wa kilimo kuweka mbinu madhubuti hususani matumizi sahihi ya pembejeo zenye ubora pamoja na ushirikiano ili kuongeza tija katika sekta ya hiyo ambayo ni mhimili mkuu wa uchumi wa Taifa na ustawi wa wananchi.

Amesema, kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Taifa kwani kinachangia takribani 30% ya pato la Taifa huku 60% malighafi zote za viwanda zikitoka kwenye sekta hiyo na inalihakikishia taifa usalama wa chakula kwa 100%.

Ameongeza kuwa kufanya kazi kwa pamoja kutaimarisha umoja na mshikamano, kuwezesha upangaji mzuri wa mikakati ya maendeleo na kuimarisha mnyororo wa thamani wa uzalishaji wa mazao kuanzia uzalishaji, uhifadhi hadi usindikaji, hatua itakayochochea ukuaji wa sekta ya kilimo na uchumi wa jamii kwa ujumla.

Aidha, Bi. Kyamani amewataka washiriki wa mafunzo hayo kutumia fursa hiyo kuhuisha na kuimarisha Chama cha Wauzaji wa Pembejeo Tanzania (TANADA) ili kiwe chombo imara cha kuwasaidia wakulima na kushirikiana na Serikali katika kutekeleza sera za kilimo.

Kwa upande wake Afisa Kilimo Mkuu kutoka Wizara ya Kilimo, Bi. Justa Katunzi amesema kuwa Serikali imeendelea kuimarisha mnyororo wa thamani wa upatikanaji wa mbegu bora kwa kuziwezesha taasisi za uzalishaji wa mbegu ikiwemo TARI, ASA na TOSCI kwa lengo la kuhakikisha wakulima wanapata mbegu zenye tija na faida kiuchumi.

Vile vile, Bi. Katunzi amewahimiza wadau wa mbegu chini ya Chama cha Wauzaji wa Pembejeo Tanzania (TANADA) kuhakikisha pembejeo bora zinawafikia wakulima walioko vijijini kwa wakati ili kuongeza uzalishaji, kuboresha kipato cha wakulima na kuchangia maendeleo ya Taifa.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RC MTANDA AMPOKEA WAZIRI DEUS SANGU MWANZA

    February 20, 2026
  • RC MTANDA AWATAKA WASIMBE NA WABANZA KUUNGANA KUKATA BIMA YA AFYA KWA WOTE

    February 20, 2026
  • RC MTANDA AZINDUA SHULE YA SEKONDARI BUMYENGEJA KWIMBA

    February 20, 2026
  • RC MTANDA AZINDUA NYUMBA YA WATUMISHI KITUO CHA AFYA BUDUSHI, ATOA WITO KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA KWA WOTE

    February 20, 2026
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.