RC MAKALLA AZINDUA MIUNDOMBINU YA KIDATO CHA TANO MWAMASHIMBA SEKONDARI, KUSAIDIA KUONDOA MSONGAMANO DARASANI NA BWENINI
*Aupongeza uongozi wa shule hiyo na Halmashauri kwa usimamizi mzuri wa ujenzi*
*Awataka wanafunzi kutumia uboreshaji wa miundombinu kusoma kwa bidii kuongeza ufaulu*
*Aagiza kulinda eneo la shule hiyo kwa kutambua mipaka na kuweka uzio*
*Awataka wazazi kupeleka watoto shule wakapate elimu na sio kuwaacha nyumbani*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla leo Novemba 28, 2023 amezindua miundombonu ya kidato cha tano kwenye Shule ya Sekondari Mwamashimba wilayani Kwimba iliyogharimu zaidi ya shilingi Milioni 600.
Akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo, Mhe. Makalla amewapongeza uongozi wa shule hiyo na halmashauri kwa usimizi mzuri wa Mabweni 3, vyumba vya madarasa 8 na Matundu ya vyoo 13 utakaosaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi kwenye madarasa na mabweni.
"Nimeona mabweni mazuri yenye mpangilio mzuri wa vitanda, madarasa na matundu ya vyoo vyote kwenye hali ya usafi na unadhifu mzuri, tumieni jitihada hizi za uboreshaji kutulia na kusoma kwa bidii na nina imani baadae tutawapata viongozi wazuri kutoka kwenye shule hii." Makalla.
Vilevile, Mhe. Makalla ameagiza kulindwa kwa eneo la shule hiyo kwa kutambua na kuweka mipaka na kuweka uzio ili kuwalinda wanafunzi na kuepusha migogoro ya ardhi inayosababishwa na wananchi kuingia kwenye maeneo ya taasisi hususani yasiyo na mipaka inayofahamika.
Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija amemhakikishia kiongozi huyo wa Mkoa kuwa ufaulu utqongezeka kwani pamoja na kuondoa msongamano wanafunzi kwenye shule hiyo watapata fursa nzuri ya kusoma kwenye mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia.
"Mhe. Mkuu wa Mkoa wanafunzi wa kidato cha tano na sita wapo zaidi ya Mia 600 lakini kwa uwepo wa mabweni haya hivi sasa kila mwanafunzi atalala kwenye kitanda chake, hakuna tena msongamano bweni wala darasani." Amefafanua Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi. Happness Msanga.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa amezindua Shule mpya ya Msingi Mwalulyeho katika kijiji cha Chasalawi, Bupamwa- Mwamashimba iliyojengwa kwa zaidi ya Milioni 250 ambayo imesaidia kuondoa adha ya kutembea umbali wa zaidi ya Kilomita 4.5 kuelekea shule ya Chasalawi.
"Kama mlikua na kiu ya kupata shule, sasa mmejengewa tumeiona ni nzuri yenye samani za kutosha, basi waleteni watoto kwenye hii shule wasome maana hawa 303 wamehamia hivyo wazazi hakikisheni watoto wote wanakuja shule ifikapo mwezi Januari 2024 asibaki nyumbani hata mmoja mweye umri wa kuanza shule. Mkuu wa Mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.