Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima leo amefanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa madarasa akianzia Wilaya za Nyamagana,Ilemela na Magu na kuhimiza ujenzi bora na kumalizika kwa wakati kabla ya mwaka huu kumalizika.
Mkuu huyo wa Mkoa akianzia ziara hiyo Wilayani Nyamagana shule ya Sekondari Mirongo amekagua ujenzi wa madarasa ya maghorofa na kutaka ofisi za walimu zisiwe mbali na madarasa hayo ili kudumisha nidhamu kwa wanafunzi na uwepo mzuri wa uwiano wa matundu ya vyoo na idadi ya wanafunzi.
"Noana maendeleo mazuri ya ujenzi wa madarasa lakini hili la ofisi za walimu kuwa mbali sijafurahishwa nalo kabisa,kila baada ya madarasa matatu lazime iwepo ofisi ya walimu ndiyo ujenzi wa kisasa ninao utaka" Mhe.Malima
"Wilaya ya Nyamagana tumepokea Shs Bilioni 3.92 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 196,ambapo 130 yatakuwa ya chini na 60 ya ghorofa na madarasa yote yapo hatua za mwisho kukamilika kabla ya Disemba hii,tunatarajia kuwapokea Januari mwakani wanafunzi wote waliofaulu mwaka huu" Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe Amina Makilagi.
Aidha Mhe Malima akiwa Wilayani Nyamagana amekagua mradi wa barabara ya Unguja A ya mita 372 iliyogharimu Shs milioni 295 chini ya Mkandarasi Nyanza Road Works ambayo utekelezaji wake umefikia asilimia 73 ukigharimiwa na mfuko wa barabara
"Sisi Wilaya ya Ilemela tumepokea Shs Bilioni 2.2 za ujenzi wa madarasa 110,tayari 88 yamekamilika na 22 yapo hatua ya ukamilishaji,mahitaji yalikuwa madarasa 252 lakini tumejenga jumla 2548"Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilemela Injinia Modest Apolinary.
Huko Wilayani Magu Mhe.Malima amefanya ukaguzi wa barabara ya Kisesa-Bujora yenye urefu wa Kilomota 1.72 inayojengwa na Mkandarasi Mangi Construction Ltd Kwa gharama ya zaidi ya Shs Bilioni 1 iliyo chini ya TARURA lakini inakabiliwa na changamoto ya uwepo wa mawe makubwa ardhini na kusua sua kwa kuondolewa nguzo za Tanesco na minara ya Kampuni za simu.
"Mmeniambia hii barabara mnatarajia kunikabidhi Mei 6 mwakani,sasa hizi changamoto nataka kesho mzizungumze kwa kina kikao cha bodi ya barabara ili nami nijue eneo langu kama Mkuu wa Mkoa nazitatuaje" amesisitiza Mkuu wa Mkoa
"Tumepokea zaidi ya Shs Bilioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 163 ujenzi upo hatua ya asimia 82 na madarasa 26 yapo hatua ya ukamilishaji na mengine yamekamilika tunatarajia Disemba 22 mwaka huu madarasa yote kuwa tayari"Mkurugenzi wa Halmashauri ya Magu Fidelica Myoveka.
Mkoa wa Mwanza umepokea zaidi ya Shs Bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa Wilaya zote zilizopo ndani ya Mkoa huo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.