Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima leo Januari 13, 2023 ameipokea Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji ikiwa ziarani kukagua Mradi mkubwa wa Maji Butimba unaosimamiwa na Mamkala ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) wenye thamani ya Bilioni 69.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Almas Maige akimuwakilisha Mwenyekiti wa kamati hiyo amesema wamefika Mwanza kukagua Mradi wa Maji wa Butimba kujionea ni kwanini mradi huo haujaanza kutoa huduma ya maji Disemba mwaka jana kama Makamu wa Rais alivyoagiza.
"Kamati hii inafanya kazi kubwa na kwa mafanikio makubwa sana na Wizara yetu imetumia sana Ushauri wa kamati hii kila wakati katika kuendeleza Sekta ya maji nchini, nakuahidi Mhe. Mkuu wa Mkoa vifaa vitafika ndani ya muda kutoka Ufaransa ili mradi ukamilike na nakuahidi kuwa tatizo la kutolewa maji kwa zamu mwanza litakwisha" Naibu Waziri wa wizara ya Maji Mhe. Maryprisca Mahundi.
Mhe. Malima ametumia wasaa huo kuwakaribisha wajumbe wa kamati hiyo na amebainisha kuwa Mradi wa Maji wa Maji Butimba ni mradi wa kimkakti kwa kuwa unakuja kutatua Changamoto kubwa ya maji na upo kama kielelezo cha Maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi na Sekta hiyo mkoani humo.
"Mahitaji ya Maji kwa watu wa Mwanza ni Lita milioni 160 na mradi wetu mkubwa unaofanya kazi kwa sasa unazalisha Lita milioni 90 na sasa ukitoa maji yanayopotea wakati wa Usambazaji ambayo ni wastani wa lita milioni 32 tunapata maji lita milioni 65 kwa siku, hivyo mradi wa Butimba ambao unatarajia kuzalisha lita Milioni 48 utakua msaada mkubwa." Amefafanua Malima.
Vilevile, amejinasibu kuwa mkoa huo unatekeleza miradi ya Maji yenye thamani ya takribani Bilioni 300 na akatoa wito kwa MWAUWASA kudhibiti upotevu wa Maji ili uzalishaji uendane na usambazaji hivyo wañanchi waondokane na kero ya upungufu wa huduma hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.