Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima amesema ni muhimu kuimarisha njia za upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi ili kuhakikisha huduma bora kwa wananchi zinatolewa kwenye vituo vya afya nchi nzuma
Hayo yamesemwa leo Mei 6 2023 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndg. Balandya Elikana kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kuhusu mfumo mpya wa mshitiri katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa.
"Ni muhimu sana kuimarisha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, vifaa saidizi na vitendanishi kulingana na mahitaji ya vituo vya afya katika ngazi zote za utoaji huduma nchini na kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa wananchi," Amesema Mtendaji huyo wa Mkoa
Ndg. Balandya ameipongeza Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambao ndio wawezeshaji wa mafunzo hayo kwa kuendelea kuboresha mfumo wa mshitiri na endapo utasimamiwa vizuri utasadia upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.
" Niipongeze Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa kuendelea kuboresha mfumo wa mshitiri na ni matumaini yangu na Serikali kuwa mfumo huu endapo utasimamiwa vizuri utasaidia katika upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi zinazokosekana katika Bohari la Dawa," Amesema Ndg. Balandya.
Aidha Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Claudia Kaluli amesema Ofisi ya Rais- TAMISEMI ikishirikiana na wizara ya afya imeleta mfumo wa uagizaji dawa ambazo zitakua hazipatikani katika Bohari la Dawa ambao ni rahisi.
" Ofisi ya Rais- TAMISEMI ikishirikiana na wizara ya afya imeleta mfumo wa uagizaji dawa ambazo zitakuwa zinakosena katika Bohari la Dawa ambao ni rahisi na utasaidia kuweza kushirikiana na wauzaji binafsi," Amesema Kaluli
"Huu ni mfumo ambao tunaimani unakuja kuleta mageuzi chanya kwenye Sekta yetu ya afya kutokana na upatikanaji wa haraka wa dawa na usahihi wa nyaraka husika",Julius Shigella,Mratibu wa huduma za Maabara na damu salama Mkoa.
Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2023 iliweka bayana na kawaahidi wananchi kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi na kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi katika utoaji wa huduma za afya.
Washiriki wa mafunzo hayo ni Wakurugenzi kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Mwanza,Waganga wakuu wa Wilaya,Maafisa TEHAMA,waratibu wa huduma za Maabara na Maafisa ugavi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.