Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima amewashauri Wataalamu wa kilimo kuendelea kuwaelimisha wakulima kuhusu teknolojia na ulimaji wa kisasa ili uwe na tija kwao wakati wa mavuno.
Akifunga Mkutano wa Kimataifa Jijini Mwanza uliokuwa ukiangalia maendeleo na utekelezaji wa mradi wa Teknolojia unaojulikana kama SKUMA VUTA unaofadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya (EU) unaolinda zao la Mahindi kushambuliwa na wadudu waharibufu, Mkuu huyo wa Mkoa amesema mageuzi bora ya kilimo yanapaswa kufuatiliwa kwa karibu kuona kama kuna changamoto zozote na kuzitatua ili mkulima atumie nguvu kidogo na kufaidika wakati wa mavuno yake.
"Niwapongeze sana wafadhili wa mradi huu wenzetu nchi jirani ya Kenya wamepiga hatua sana katika kilimo cha Mahindi kutokana na kutumia teknolojia kama hii, naamini Tanzania muda mfupi ujao tutapiga hatua kubwa hasa kutokana na ukubwa wa ardhi yetu yenye rutuba." Mhe.Malima
Amebainisha kuwa sherehe za Nanenane zinazofanyika kila mwaka Mkoani Mwanza zitumike kikamilifu kama jukwaa la kuwaelimisha wakulima kuhusu mageuzi hayo chanya ya Kilimo ambayo yatakuwa mkombozi kwao kiuchumi..
"Tumefika hapa Tanzania ambapo mimi ni mara yangu ya kwanza kujionea maendeleo ya mradi huu,wakulima watumie fursa hii kupata uelewa na sisi tupo kwa ajili ya kuwasikiliza ili mwisho wa siku tufike katika malengo yetu ya ulimaji wa kisasa wa kupata mazao bora na ya kutosha" Prof.Emily Poppenborg, Mratibu wa mradi UPSCALE.
"Mradi huu wa miaka mitano hapa kwetu sasa ni mwaka wa pili na miezi minne,unatekelezwa nchi tano barani Afrika zikiwemo Kenya,Uganda,Rwanda na Ethiopia na tumelenga zao la Mahindi kutokana na kuwa ni la usalama kwa chakula" Dkt.Paul Saidia Mkurugenzi TARI
Mradi wa SKUMA-VUTA ni teknolojia ya kupanda mimea wa jamii ya mikunde kwenye shamba la mahindi ambayo inazuia wadudu waharibufu kama Viwavijeshi kushambulia zao hilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.