Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Wilaya ya Ukerewe amefanya Ziara ya Kikazi kisiwa cha Irugwa na Gana kukagua miradi ya maendeleo.
Akiwa Kisiwani Irugwa ametembelea shule ya Sekondari Irugwa ili kujionea miundombinu na hali halisi ya shule hiyo iliyokamilika ujenzi wa vyumba 6 vya madarasa 2021 vyenye thamani ya shilingi milioni 120.
Aidha, Mhe.Malima ameshiriki chakula cha mchana na wanafunzi wa shule hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa zawadi ya shilingi laki tatu na thelathini (330,000) na kuahidi kuwapatia wanafunzi wa kidato cha nne Shilingi milioni 1 zitakazowasaidia kipindi cha mitihani, pamoja na Jezi za kiume na kike pamoja na mipira 2 kwa wasichana na 2 kwa wavulana.
Baada ya kukamilisha Ziara yake Kisiwa cha Irugwa Mhe.Malima na Kamati ya ulinzi na usalama alielekea Kisiwa cha Gana Kijiji cha Kamasi,Kata ya Ilangala na kukagua Ujenzi wa Zahanati na kuwapongeza wananchi kwa kuchangia Shughuli milioni 8 kwa ajili ya kununua eneo hilo lenye ukubwa wa mita 50 kwa 60 na kuwataka waendelee kujitoa ili kufanikisha ujenzi huo.
Pamoja na wananchi kuonesha kuunga mkono juhudi za Serikali kuwasaida wananchi wake Mhe.Malima yeye binafsi amechangia ujenzi wa Zahanati hiyo shilingi milioni 1 pamoja na mfuko wa Mkuu wa Mkoa utachangia Shilingi milioni 1 na kuwataka wadau mbalimbali kuendelea kuchangia ili kufanikisha ujenzi huo.
"Serikali uwa inatoa milioni 50 pale ambapo kuna nguvu za wananchi zimeonekana, nendeni mkachangishane kuipa nguvu Serikali ya kuwashika mkono," amesema Mhe.Malima.
Hata hivyo,Mhe Malima ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kutatua Changamoto mbalimbali zinazokwamisha utekelezaji wa miradi katika Wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na maeneo hayo ya visiwani aliyoyatembelea bila kusahau upandaji wa miti ili kutunza mazingira.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.