Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amefungua kikao cha kwanza cha bodi ya barabara ya Mkoa kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambacho kimeudhuriwa na wajumbe zaidi ya 38.
Katika kikao hicho Mhe Mongella alimuagiza Meneja wa Mkoa TEMESA kuhakikisha vyoo vinajengwa kwenye vivuko vyote vinavosimamiwa na TEMESA.
"Vyoo vijengwe kwenye vivuko vyote vinavyosimamiwa na TEMESA, kufikia tarehe 15 mwezi wa 12 viwe vimekamilika"alisema Mhe. Mongella.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Kikao cha bodi ya barabara Mhe Richard Ndasa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sumve, alishauri mamlaka ya bandari kubaini bandari bubu kwakuwa Mkoa si salama sana kulingana na kupakana na nchi jirani.
"Bandari bubu zinamambo mengi, kama tutashindwa kuzibaini ipo siku tutapata matatizo. Ikiwezeka wahusika waweke cctv camera ili kubaini kinachoingia, kilichobebwa na aliyekibebe" alisema Mhe. Ndasa.
Hata hivyo, Kaimu Mkuu wa bandari ziwa victoria Morris Mchindiuza alisema kuna bandari bubu 143 katika ziwa victoria huku bandari zinazopatikana ukanda mzima sita.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.