Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella ameipongeza Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira ya jijini Mwanza ( MWAUWASA) kwa kutekeleza vyema mradi wa ujenzi wa tenki la majisafi katika mji wa Ngudu wilayani Kwimba.
Mradi huo wa tenki la kuhifadhia maji unagharimu zaidi ya million 490 ( 490,845,470.84) ambazo zinatolewa na serikali kupitia Wizara ya maji ambapo ujenzi wake unatarajia kukamilika Agosti mwaka huu.
" Hongera sana Kaimu Mkurugenzi wa MWAUWASA Mhandisi Leonard Msenyele mnafanya kazi nzuri kwa manufaa ya wananchi kweli inapendeza imani yangu wananchi watanufaika nao ipasavyo" anasema Mhe. Mongella.
Naye Mhandisi wa maji MWAUWASA Chacha Mwita alieleza kuwa wastani wa utekelezaji wa kazi zote za ujenzi tenki hilo lenye lita za ujazo 2,000,000 umefikia asilimia 80.
" Tenki hili linapata maji kutoka KASHWASA na linategemewa kuhudumia wakazi wapatao 37,000 wa mji wa Ngudu" alieleza Mwita.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.