"Benjamin Mkapa, alikuja na sera ya uwazi, ukweli ili kuhakikisha tumeingia kwenye uchumi wa soko ambapo mifumo thabiti ya kudhibiti nguvu za soko na kuweka mifumo ya kisasa ya utendaji kazi,"
Hayo ni maneno ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella alipokuwa akimzungumzia aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya tatu ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia July 24 mwaka huu alisema katika uendeshaji wa serikali marehemu alihakikisha uimarishaji wa sekta binafsi,ubinafishaji wa mashirika na kuleta ufanisi kwenye uchumi.
Alisema kuondoka kwa Mkapa ni pigo kwa taifa ,kwani wakati wake alisimamia sana kuimarisha mifumo ya kiserikali,na ukienda katika maeneo mbalimbali alifanya mambo mengi ambayo yaliwagusa watu moja kwa moja .
" Ukienda Ukerewe ile Mv Nyerere ni yeye ndiye aliridhia itengenezwe , alitengeneza vitu vingi sana ikiwemo kupeleka Umeme ,miradi ya maji katika maeneo mengine mengi ulitengenezwa wakati wake Mwanza tuna historia kubwa na Mzee Mkapa ni mtu ambaye amechangia sana kwenye maendeleo ya nchi yetu" alisema Mongella.
Aliongeza kuwa kila awamu ya uongozi wa nchi hii inafanya mambo ya msingi kwenye kuimarisha na kufanya maboresho katika jamii ambapo wakati wa Mwalimu Nyerere misingi ya nchi ilijengwa na uzalendo ulikuwa wa kiwango cha juu,hivyo ni wakati wetu kujiombea ili tuweze kuimarisha misingi na kuiga mifano mema ambayo wazee wetu wameiweka akiwemo Mkapa.
"Nikikumbuka naumia sana Mwaka huu tu February 21 tulikuwanaye kwenye mkoa wetu takribani siku tatu ,alitupa heshima kubwa sana yeye na ofisi yake baada ya kuzindua kile kitabu chake Cha My life my purpose Dar, es salaam kituo Cha pili alipokuja kukitambulisha kitabu kile ilikuwa Mwanza na alipokuwa akizungumza aliongea maneno mazito" alieleza Mongella.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.