RC MTANDA AAGIZA
MAAFISA POLISI WANAOKIUKA SHERIA KUCHUKULIWA HATUA.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Said Mtanda amewataka maafisa Polisi mkoani humo wanaotenda kazi kinyume na utaratibu wa sheria za nchi zilizoainishwa kuchukuliwa hatua mara moja ili kukomesha uchafuzi wa taswira ya jeshi la Polisi.
Ameyasema hayo leo Julai 6,2024 alipohudhuria hafla fupi ya utoaji wa sifa na zawadi kwa wakaguzi na askari tisa waliofanya vizuri kwa kipindi cha mwaka 2023/2024 iliyofanyika katika uwanja wa Polisi FFU Mabatini.
“Askari wote mliopo hapa muendelee kuimarisha nidhamu na wale wachache ambao wanaoonyesha nidhamu ambayo siyp sahihi kwa jeshi la polisi wachukuliwe hatua kwakuwa wanachafua taswira ya Jeshi la Polisi.” Mtanda
Mtanda ameongeza kwa kusema askari Polisi na watumishi wote wa mkoa wa Mwanza kuzingatia weledi katika kazi na kuepuka na kuacha kujihusisha na vitendo vya kupokea rushwa.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbroad Mtafungwa amesema anawashkuru sana wananchi kwa kutoa msaada mkubwa kupitia mkakati wa Jeshi la Polisi wa kuishirikisha jamii katika kuzuia uhalifu kushirikiana na Polisi kuweza kuyafichua maovu yanayofanywa na waharifu.
“Hali ya ulinzi na usalama mkoani Mwanza ni shwari hakuna matukio makubwa yanayohatarisha usalama wa wananchi na mali zao jeshi la polisi kushirikiana na wananchi wanafanya msako kuzuia uharifu Mwanza”. Mtafungwa
Baadhi Wananchi wamejitokeza kushuhudia hafla hiyo fupi na kuweza kupewa nafasi mbalimbali kama kusoma shairi la kupongeza ufanisi na utendaji bora wa Jeshi la Polisi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.