Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewakumbusha Wadau wa Afya Wanaohudumiwa na MSD Kanda ya Mwanza kuwa wana jukumu kubwa la kuvisimamia vituo vya kutolea huduma za afya katika maeneo yao ili viweze kukusanya mapato ya kutosha.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo leo wakati akifungua Mkutano wa mwaka na wadau wa sekta ya afya ambapo amewataka kusimamia mapato yanayotokana na uchangiaji wa huduma za afya ili yaweze kununua bidhaa za afya, sambamba na kusimamia mnyororo wa ugavi wa bidhaa hizo.
Mhe. Mtanda amesema Serikali ya awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuongeza kiasi cha fedha inayotengwa kwa ajili ya bajeti ya kununulia bidhaa za afya kwa ajili ya vituo vya kutolea Huduma za Afya ili kuboresha utoaji wa huduma za afya.
“Hivyo, kila mmoja ana jukumu la kusimamia matumizi sahihi ya bidhaa za afya ili Kuleta tija kwa wananchi.”
Kwa kutekeleza haya, wananchi watapata huduma bora zaidi katika vito vya kutolea huduma za Afya bila manung’uniko. Ameongeza Mkuu wa Mkoa.
Kupitia mkutano huo Mkuu wa Mkoa pia amewakumbusha wadau wa MSD kupitia Wizara ya Afya, kufanya maoteo ya bidhaa za afya kwa usahihi, weledi na kwa wakati.
Kadhalika, amewakumbusha kusimamia matumizi sahihi ya takwimu za mnyororo wa ugavi ili ziwasaidie kufanya maamuzi sahihi juu ya bidhaa za afya
Katika maeneo yeo.
Mkutano huo wa MSD na wadau wa afya wa Mikoa mitano ya Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Mara na Geita wanaohudumiwa na Kanda ya Mwanza una madhumuni ya Kuboresha uhusiano na mawasiliano kati ya MSD na wadau wa Afya katika mikoa ya Kanda ya ziwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.