RC MTANDA AIPOKEA KAMATI YA BUNGE YA PIC MWANZA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo tarehe 21 Machi, 2025 ameipokea Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma iliowasili kwa ziara ya siku 3 katika kukagua miradi mbalimbali ambayo Serikali imewekeza fedha.
Akiongea katika kikao kifupi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mhe. Mtanda amewashukuru kamati hiyo kwa kuja kukagua maendeleo ya ujenzi wa upanuzi wa bandari ndani ya Mkoa huo kwani watasaidia kuchagiza kasi ya ukamilishwaji.
"Mmefanya vizuri kuja kukagua mradi wa upanuzi wa bandari zetu za Mwanza Kaskazini na Kusini ambazo zipo kwenye upanuzi kufuatia ujenzi wa Meli kubwa ya kisasa iliyofikia zaidi ya asilimia 90 na itakapoanza kazi kupitia bandari hizo basi tuna uhakika safari za Bukoba, Jinja na Kampala."
Aidha, amebainisha kuwa ukamilifu wa miradi ya bandari pamoja na daraja la Kigongo - Busisi utasaidia kukuza uchumi wa Mwanza na kupelekea kuongeza pato la Taifa kutoka Mwanza ambalo kwa sasa ni Trilioni 13.5 sawa na asilimia 7.2 ikiufanya Mkoa huo kushika nafasi ya pili kwa uchangiaji ukitanguliwa na Dar es Salaam.
Vulevile, amebainisha kuwa Mwanza kuna chanzo cha maji kizuri cha Butimba chini ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (MWAUWASA) chenye pampu mpya 3 na kwamba zaidi ya Lita Milioni 48 zinazalishwa kwa siku kupitia chanzo hicho ambacho kinafanya Mwanza kuwa na uhakika wa maji.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye ni Mbunge wa Kasulu Mhe. Augustino Vuma amesema wamekuja Mwanza kukagua miradi ya Maji, Bandari na Daraja ili kuona kama kuna tija ya uwekezaji uliofanywa na Serikali kwa fedha nyingi pamoja na kuona kama taratibu za matumizi ya fedha zimefuatwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.