RC MTANDA AISHUKURU MAHAKAMA KUTOA ELIMU YA RASIMU DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewashukuru wadau wa Mahakama na Taasusi zote zinazosimamia haki madai kwa kushiriki kikamilifu katika utoaji wa elimu kwenye masuala ya kisheria na rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050.
Mhe. Mtanda, ametoa shukrani pia kwa Serikali chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa maendeleo na kutoa nafasi ya pekee kwa wananchi na wadau kushiriki kikamilifu mchakato mzima wa maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo hadi pale itakapokamilika.
Mhe. Mtanda amesema hayo leo Februari 03, 2025 alipokuwa akitoa salamu za Mkoa katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria Nchini yaliyoadhimishwa Kikanda katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Mwanza Wilayani Ilemela.
“Sote tunafahamu ya kwamba mchakato wa uandaaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo hupitia hatua mbalimbali zinazohusisha wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo, ikiwemo utoaji na upokeaji wa maoni kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali zikiwemo taasisi zinazosimamia haki madai nchini”.
Hivyo, nina imani kupitia elimu mliyotoa kwa wananchi kuanzia tarehe 25 Januari, 2025 hadi leo wamepata uelewa wa kina kuhusiana na Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050. Ameongeza Mhe. Mtanda.
“Kwa lugha rahisi zaidi, Dira ya Taifa ya Maendeleo ni picha au maono
kuhusu mustakabali tarajiwa wa maendeleo ya nchi katika siku za usoni”. Amesema Mhe. Mtanda
Naye, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Masijala Ndogo ya Mwanza, Mhe. Dkt. Ntemi Nimilwa Kilekamajenga ametoa rai wananchi na wadau kushiriki kikamilifu mchakato mzima wa maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo hadi pale itakapokamilika. Kwa kuwa Dira ndio imebeba maono na matarajio ya Watanzania kwa miaka 25 ijayo.
Maadhimisho ya wiki na siku ya sheria yameongozwa na kauli mbiu
inayosema:- “Tanzania ya 2050: Nafasi ya Taasisi Zinazosimamia Haki Madai Katika Kufikia Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.