Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amekabidhi Magari kwa jeshi la polisi la Mkoa huo yenye thamani ya zaidi ya Tshs. Bilioni 1.3 yatakayotumika na Mkuu wa Makosa ya jinai Mkoa, Mkuu wa Kikosi cha kutuliza Ghasia na Sita kwa wapeleelzi na Makosa ya jinai wa Wilaya.
Akikabidhi leo Septemba 12, 2025 katika viwanja vya jeshi la polisi mabatini wilayani Nyamagana ikiwa ni sehemu ya mpango kazi wa kutekeleza ahadi za Mhe. Rais za kuboresha jeshi hilo amewataka kutumia magari hayo kulinda amani na sio kutishia wananchi.
Aidha, amelitaka jeshi hilo kuendelea kufuata sheria na kanuni zao katika kukamata, kupeleleza na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wenye makosa bila uonevu.
"Jeshi la polisi ni jeshi muhimu sana, wananchi wakiliamini ni kielelezo cha uimara wa taifa na kwamba hawatakiwi kukata tamaa kufuatia kutowaamini hivyo kasimamieni sheria na sio kutisha watu." Amesema Mhe. Mtanda.
Vilevile, amelitaka jeshi hilo kujiendeleza kitaaluma, kufanya mafunzo, kufuata taratibu, sifa na uweledi wa kusimamia jeshi la polisi kwakua ndio vitu ambavyo vitasaidia katika kupandishwa vyeo pamoja na kujiendeleza huku akisisitiza kutumia vifaa walivyopatiwa kuimarisha usalama na ulinzi.
Pia, amempongeza Kamanda Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa Wilbroad Mutafungwa kwa kutekeleza majukumu yake hasa kuhakikisha nidhamu kwa kikosi chake na utulivu kwa mkoa wa Mwanza tangu kuanza kampeni za uchaguzi.
Naye, Kamanda wa Polisi Mkoa Afande Wilbroad Mutafungwa amebainisha kuwa magari hayo yatasaidia kudhibiti shughuli za uhalifu kwa kiasi kikubwa kwani vitendea kazi hivo vimeongeza utendaji Kazi kwa jeshi hilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.