RC MTANDA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI KUTOKA JIMBO LA HENAN,CHINA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Gavana kutoka Jimbo la Henan kutoka nchini China,Mhe. Liu Yujiang na kusema mahusiano baina ya Tanzania na China yamezidi kuwa na tija siku hadi siku.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo Septemba 6,2024 kwenye ukumbi mdogo wa Ofisi ya mkuu wa mkoa ukiwajumuisha Menejiment kutoka pande zote mbili,Mtanda amesema historia ya ushirikiano baina ya Mataifa hayo ni ya muda mrefu na ujio wao utazidi kukuza mahusiano kati ya Mwanza na Jimbo la Henan.
"Ziara yenu ya siku tatu hapa nchini itaongeza tija katika sekta mbalimbali ambazo tumekuwa tukishirikiana yakiwemo masuala ya teknolojia na pia tutabadilishana uzoefu wa kitaalamu kwa maendeleo ya miji yetu",Mkuu wa Mkoa.
Mtanda amebainisha moja ya shabaha kuu ya ziara yao itakuwa ni kutupatia uzoefu wa namna gani mapinduzi na mafanikio ya teknolojia kutoka Jimbo la Henan yatakavyoweza kusaidia Mkoa wa Mwanza katika baadhi ya maeneo kama viwanda na madini na tutakuwa tayari kujifunza kutoka kwao.
Katika mazungumzo hayo yaliyokwenda pamoja na kusaini barua ya kusudio iliyosainiwa na kaimu Katibu Tawala wa mkoa Ndugu Kusirie Swai na mjumbe mmoja aliyeambatana na msafara wa Naibu Gavana huyo,Mtanda ameonesha matumaini ya muendelezo wa ushirikiano huo ambao utazidi kuwanufaisha wananchi kimaendeleo kutoka pande hizo mbili kwa kuibuka fursa mbalimbali za kiuchumi.
Naibu Gavana Mhe.Liu Yujiang amesema licha ya Taifa lao kupiga hatua kubwa kiuchumi Duniani lakini wanajivunia uhusiano na Tanzania na utazidi kudumishwa ili kila upande unufaike katika nyanja zote za kimaendeleo
Waasisi wa muungano wa ushirikiano baina ya Mataifa hayo ni Rais wa awamu ya kwanza wa Tanzania, Hayati Julius Nyerere na Hayati Mao Tsetung kutoka China.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.