Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Desemba 29, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu waziri wa mifugo na uvuvi Mhe. Ng’wasi Kamani (MB) ambaye amewasili mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi katika wilaya za Sengerema, Misungwi na Nyamaganana.

Katika mazungumzo yao Mhe. Mtanda amesema katika ziara hiyo ya Mhe. Kamani ataweza kuifahamu sekta ya mifugo na uvuvi katika mkoa huo na namna ambavyo inachangia katika pato la taifa na Mkoa kwa ujumla.

Naye Mhe. Kamani Amesema ujio wake Mkoani humo unalenga kuzitembelea taasisi mbali mbali zinazojihusisha na mifugo na uvuvi pamoja na kuzitambua changamoto na mafanikio ya sekta hiyo ili kuweza kuzitaua na kuleta maendeleo.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.