RC MTANDA AMFARIJI MWENYEKITI WA CCM MKOA KUFUATIA KIFO CHA BABA MZAZI
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Desemba 31, 2024 ameshiriki ibada ya mazishi ya Baba wa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza Ndugu Michael Lishinge (SMART) katika Kijiji cha Tabaruka Wilayani Sengerema yaliyokuwa makazi ya Mzazi huyo na kuifariji familia hiyo iliyoondokewa na mpendwa wao.
Akitoa salamu za rambirambi Mhe. Mtanda ametoa pole kwa Mwenyekiti huyo pamoja na familia yake na kuwataka kumtegemea Mungu katika kipindi kigumu wanachopitia.
Aidha ametoa rai kwa wananchi waliojitokeza katika mazishi hayo na Wanamwanza wote kuishi kwa kumtemegemea Mungu kwa kuwa hakuna aijuaye kesho yake, hivyo amewataka kuishi kwa amani na upendo.
Akizungumza kwa niaba ya familia Ndugu Michael Lushinge ametoa shukrani za dhati kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa ushirikiano aliouonesha katika kipindi chote cha msiba huo yeye pamoja na Ofisi yake (akiwemo Katibu Tawala Mkoa, Bwana Balandya Elikana) aidha amesema ataendelea kuyaenzi yale mema yote aliyoachiwa na marehemu baba yake.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.