RC MTANDA ATAKA TATHMINI KUBAINI THAMANI HALISI ENEO LINALOLALAMIKIWA NA THEREZA MABULA ILI KUPATA SULUHU
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amemuagiza Kamishna wa Ardhi Mkoa kumuelekeza mthamini wa ardhi kufanya tathmini ya eneo linalolalamikiwa na Bi. Thereza Mabula lililopo mtaa wa Kanyerere ili kubaini kama baraza la ardhi la Wilaya lina mamlaka ya kusuluhisha kesi ya nsingi ya uvamizi
Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa agizo hilo leo Junu 11, 2024 alipofanya ziara kwenye eneo la Kanyerere wilaya ya Nyamagana ambapo alifanya mkutano na wananchi wa eneo hilo wapatao zaidi ya Kaya 200 wanaotakiwa kupisha kwenye eneo hilo kutokana na ushindi aliopewa Bi. Thereza mwaka 2017 na baraza la kata.
"Sheria za sasa za ardhi zimeondoa mamlaka ya kuhukumu kwa baraza la ardhi la jata bali linatakiwa kusuluhisha tu na endapo watafikisha shauri kwenye ngazi ya Wilaya basi hukumu itatolewa kwa kesi isiyozidi madai ya milioni 300 lakini hapa kuna kazi ya kufanya." Mkuu wa Mkoa.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi waliotakiwa kuondoka kwenye eneo hilo kwenda kwenye baraza la ardhi wapate ufafanuzi wa kisheria kama wanahusika na hukumu ya ushindi alioupata Bi. Thereza dhidi ya Bwana Paul Ngesera uliomtaka kuwaondoa wote kwenye eneo hilo au la.
Mwenyekiti wa baraza la ardhi la Wilaya Paulo Lekamoi amesema mgogoro huo wa ardhi ulianza kwenye kata mwaka 2009 kwa Bi Thereza kumlalamikia bwana Paul Ngesera kuvamia eneo lake Kanyerere ambapo mwaka 2017 kesi iliisha na alipewa ushindi na mwaka 2018 alifungua shauri baraza la ardhi na nyumba wilaya kwa ajili ya kukaza hukumu ya ushindi wa baraza la kata ambapo alipewa dalali kwa ajili ya kufanya utekelezaji.
Amefafanua kuwa, changamoto za utekelezaji wa agizo hilo lilikakwama maana tayari kulikua na makazi ya wananchi zaidi ya 200 ambapo ni ngumu kuwaondoa wote ili kumpatia eneo lake Bi Thereza kwani wengine hawakua ndani ya shauri lake na kupekekea Mhe. Waziri wa ardhi kumuagiza arudi mahakamani kiwashitaki wengine ili nao wasikilizwe.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.