Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewaomba radhi wananchi wa mkoa huo juu ya changamoto ya ukosekanaji maji iliyojitokeza kuanzia tarehe 19 Septemba, tatizo ambalo lilitokana na kuyumba kwa umeme katika chanzo cha maji Butimba.
Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Septemba 23, 2025 ofisini baada ya kusikiliza kero za wananchi zoezi ambalo linafanyika kila siku za jumanne.
Mhe. Mtanda amesema tayari mamlaka husika imeshaanza kushughulikia tatizo hilo ambalo mpaka sasa ukarabati umefikia asilimia 80 na baadhi ya maeneo tayari maji yameshaanza kutoka.
"Sasahivi tumefikia asilimia 80 ya marekebisho ya mitambo iliyopata athari kwahiyo kuanzia leo maji yataanza kutoka katika baadhi ya maeneo" Amesema Mhe. Mtanda.
Aidha Mhe. Mtanda amesema serikali ipo kwenye mchakato wa kupanua mradi wa maji wa Capripoint uliofikia asilimia 35 mpaka sasa ambao ulikua ukizalisha maji Lita Millioni 90 na baada ya marekebisho utazalisha maji Lita Millioni 138.
"Tunaendelea na upanuzi wa mradi wa maji na miundombinu ambapo tunaomradi wa maji wa Capripoint ambao ulikua ukizalisha maji Lita Millioni 90 na baada ya marekebisho utazalisha maji Lita Millioni 138 kwa sasa tupo asilimia 35 ya marekebisho yake.
Mamlaka ya maji mkoa wa Mwanza (MAUWASA) ilitoa taarifa kwa wananchi wa maeneo ya Mkuyuni, Nyegezi, Mkolani na Msituni juu ya upungufu wa maji katika chanzo cha maji Butimba ambao ulitokana na kuyumba kwa umeme, mradi huo unauwezo wa kuzalisha maji lita Millioni 48.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.