RC MTANDA AWAAGIZA RUWASA KUSAMBAZA MAJI KWA WANANCHI WANAOZUNGUKA CHANZO CHA IHELELE
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewaagiza Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) kuhakikisha wanasambaza maji kwa wananchi zaidi ya elfu mbili wanaoishi kwenye vijiji vya Nyangh'omango, Mbalama na Isesa vilivyopo kwenye Kata ya Ilujamate.
Mhe. Mtanda ametoa agizo hilo leo Juni 07, 2024 alipofanya ziara kwenye chanzo kikubwa cha maji cha Mamlaka ya Usambazaji Maji Kahama -Shinyanga (KASHWASA) kinachozalisha zaidi ya Lita Milioni 67 kwa siku kilichopo wilayani Misungwi.
Mtanda amesema, ni vibaya kwa vijiji vinavyozunguka mradi ambao ndio walinzi wa mradi kutopata maji safi na salama wakati mradi huo mkubwa wenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 900 ukisafirisha maji hadi kwenye mikoa ya Shinyanga, Tabora na Singida.
Kwa upande wake, Meneja RUWASA Marwa Kisibo amesema hadi kufikia Agosti mwaka huu wananchi wa vijiji hivyo watapata maji kwani kuna mradi wa usambazaji unatekelezwa na akatoa wito kwa wananchi kujiandaa kuvuta maji kwenye makazi yao kwa gharama nafuu.
"Uwepo wa mradi mkubwa kama huu ni lazima uwanufaishe wananchi wanaoishi jirani na sio kuwa wasindikizaji tu, nisikilizeni RUWASA nataka mradi wa usambazaji maji ufanyike kwa haraka ili wapate maji." Mkuu wa Mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.