RC MTANDA AWAHIMIZA VIJANA UMUHIMU WA KUCHAPA KAZI KATIKA KUJILETEA MAFANIKIO
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka vijana Mkoani humo kuhakikisha wanafanya kazi kwa hali na mali ili waweze kufikia malengo na mafanikio waliyo jiwekea.
Akiongea leo Juni 15, 2024 wakati alipotembelea shindano la kusaka mzalendo namba moja kwa nchi yake mwenye kujua Rais Samia amefanya nini katika Mkoa wa Mwanza (Samia Challenge) Mtanda amesema haamini katika njia nyepesi ya mafanikio, hata ukuu wa Mkoa, siamini kutumia ukuu wangu wa Mkoa kuniondolea umaskini wangu.
"Kwa hiyo ukitaka njia rahisi kupitia ukuu wa Mkoa basi utataka kula rushwa utawaonea watu ili upate pesa ununue ghorofa, ununue gari zuri uwe na maisha mazuri mwisho wa siku hata safari hii ya ukuu wa Mkoa itakuwa safari fupi." Amesema RC Mtanda.
Aidhe, Mhe. Mtanda amewataka Vijana hao kukaa mbali na tamaa kwani sio kila kitu wanavyo vitamani wanaweza kuvipata, hali inayoweza kuwapelekea kuishia pabaya na wakashindwa kufikia mafanikio na malengo waliyojiwekea kwa sababu ya tamaa.
Akiongelea maadili, Mhe Mtanda amewataka vijana wa kike kutokubali kutumika vibaya au kununulika kwa kuelewa na kutambua thamani yao, kwa kuweka jitihada katika mambo wanayoyafanya na Mungu atawasaidia kwa sababu kwenye nia pana njia.
"Katika jambo ambalo nikikutana na Vijana napenda kuwausia ni umuhimu wa kujali na kutunza afya zao, hakuna maendeleo wala mafanikio bila ya afya bora, huwezi kutimiza ndoto zako za maisha kama afya haiko sawa sawa, lakini pia afya ikishayumba utatumia fedha na muda mwingi katika kushughulikia afya zetu. Ameongeza Mhe. Mtanda.
Mtanda kadhalika amewataka Vijana hao kuhakikisha wanatenga muda wa kufanya mazoezi na kujiepusha na vitu vinavyoweza kuharibu afya ikiwemo uvutaji wa sigara, bangi, ulevi na matumizi ya dawa za kulevya, ngono zembe na vitu vyote vinavyochochea uharibifu wa afya.
Akihitimisha hotuba yake Mkuu huyo wa Mkoa amewapongeza vijana hao kwa ushiriki wao, aidha amesema hapa Mwanza Serikali ya Rais Samia ipo imara chini ya uongozi wake kama Mkuu wa Mkoa na amewataka vijana hao pia kuendelea kuiunga mkono Serikali ya awamu ya sita kwa kufanya kazi kwa bidii.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.