RC MTANDA AWAPONGEZA NBC KWA IFTAR YA USHIRIKIANO
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameipongeza Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Mkoani Mwanza kwa kuandaa iftar maalumu kwa ajili ya Wafanyakazi kutoka benki hiyo na Wadau ikiwa na lengo pia la kukumbushana ufanisi na maboresho yaliyofanywa katika huduma.
Mhe. Mtanda amesema kwa kawaida shughuli ya kufturisha inafahamika ni kwa ajili ya wale wenye uhitaji lakini benki ya NBC wao wameamua kuimarisha mahusiano kwa kuwakutanisha wadau wao na kufturu pamoja.
Aidha Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi wa mkoa wa Mwanza kuiunga mkono benki hiyo ya Taifa kwa kuwa Serikali nayo ina hisa katika benki hiyo, hivyo kutokana na ruzuku zinazotolewa ndipo Serikali nayo inapata kutekeleza miradi yake mbalimbali.
“Ukifanya miamala kupitia benki hii, unakuwa mzalendo, unachangia maendeleo ya mkoa na Taifa lako”.
Naye Meneja wa Benki hiyo Bw. Thomas Lijaji amesema wanajivunia kushiriki na wadau wao katika tukio hilo la kidini ambapo ni kwa mara ya kwanza kufanya hivyo kwa mkoa wa Mwanza.
Iftar hiyo imewakutanisha viongozi wa benki ya NBC na watumishi wao, viongozi wa Dini pamoja na wadau mbalimbalo wa Benki hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.