RC MTANDA AWASILISHA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM KWA HALMASHAURI KUU ILIYOSHEHENI MAZURI
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Mei 31, 2024 amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha Januari 2021 hadi Disemba 2023 kwa Halmashauri kuu ya Chama hicho iliyosheheni ya kujivunia yaliyofanywa ndani ya miaka mitatu.
Mhe. Mtanda amesema pamoja utekelezaji wa miradi lukuki katika Sekta za Afya, Maji, Miundombinu na Elimu, Mkoani Mwanza Serikali imeajiri watumishi 2697 kwenye sekta mbalimbali na Bilioni 2.5 zimetumika kulipa stahiki na kwamba inaendelea kuboresha utumishi kwa kujenga ofisi na makazi hadi kutumia Bilioni 16 Mwanza.
"Katika kuboresha Elimu ya awali kwa shule za Msingi Madarasa 53 ya mfano yamejengwa ndani ya miaka mitatu na walimu wa awali wameajiriwa hadi kufikia 979 kutoka 923 waliokuwepo awali na uandikishaji wa wanafunzi umeongezeka kutoka shule 1048 hadi 1118 sawa na ongezeko la shule 70 mpya", Mhe. Mtanda.
Ameongeza kuwa pamoja na miradi kama SEQUIP, BOOST na mingine Serikali imeendelea kuboresha masuala mazima ya Elimu hadi Elimu ya Juu hususani kwa ujenzi wa miundombinu pamoja na utoaji wa mikopo ya Elimu ya juu kwani Bilioni 136 zimetolewa kwa wanafunzi zaidi ya Elfu 40.
Katika sekta ya afya amebainisha kuwa ujenzi wa zahanati umeongezeka kutoka 274 hadi 319 na kwamba 385 zimejengwa kwenye Mamlaka za Serikali za mitaa na afua za lishe zimetengwa zaidi ya Bilioni 1 kwa ajili ya kujenga jamii yenye afya na Siha njema na vifo vya wazazi mwaka vimezidi kushuka.
Kupitia RUWASA Serikali inatekeleza miradi 38 yenye thamani ya Bilioni 112 ambapo 40 ya Bilioni 24 imekamilika na Serikali imepokea seti ya mtambo wa kuchimba visima na mradi mkubwa wa Kapripoint unapanuliwa na kuongezewa nguvu na mradi wa Butimba na usambazaji ndio dira mkononi kwa sasa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Mhe. Michael Lushinge amempongeza Mkuu wa Mkoa kwa kufanikisha uwasilishaji wa Ilani hiyo kwani amefikia takwa la kisheria na kufanikiwa kutoka kwenye ukwamo wa uwasilishaji huo uliodumu kwa miaka mitatu.
Mhe. Lushinge amesema siku za karibuni wamekagua miradi 31 yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 200 na ametumia wasaa huo kumpongeza Mtendaji Mkuu wa MWAUWASA kwa kutekeleza kwa vitendo sera ya kuwaletea wananchi maji na hakuacha kumsifu Meneja RUWASA wa Ukerewe Mhandisi Zubeda Saidi kwa kukamilisha miradi na kubakisha nilioni 320 zilizosaidia kusambaza maji kwenye Vijiji nje ya mradi.
Halikadhalika, Halmashauri hiyo imeshauri Serikali kuweka mkazo kulisemea zao la Pamba kwani ndio linategemewa kwenye uchumi wa Mwanza na wakatoa wito kwa Sekta ya Uvuvi kuzingatiwa ili ikuze pato la wafanyabishara na ili kulinda mazalia ya Samaki wamesisitiza kuandaliwa kwa mipango ya kuzuia uvuvi haramu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.