RC MTANDA AWATAKA MAAFISA UHAMIAJI NA ASKARI KUWA NA NIDHAMU, KUEPUKA RUSHWA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Juni 3, 2024 amehudhuria hafla ya kuvishwa nishani Maafisa Ukaguzi na askari 203 kutoka Jeshi la Uhamiaji na kuwataka kutanguliza nidhamu na kuepuka rushwa kazini.
Akizungumza na Maafisa hao kwenye viwanja vya Ofisi ya Uhamiaji Mkoa, Mtanda amebainisha hatua ya Rais kuwavisha nishani hizo ni kutokana na sifa walizonazo hivyo wanapaswa kuwa mabalozi wazuri kwa wengine.
"Nawapongeza sana kwa hatua hii, kumbukeni si jepesi hili na ndeleeni kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ili mtoe huduma bora kwa wananchi", Mkuu wa Mkoa.
Amesema kila eneo la kazi lina changamoto zake na Serikali inazitatua kadiri ya uwezo wake na akawataka Maafisa hao kusimamia vizuri usalama wa nchi kwa watu wanaoingia na kutoka.
Amempongeza pia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala kwa kuridhia hafla hiyo kufanyika mkoani Mwanza na kusisitiza Mkoa huo ndiyo kitovu cha biashara eneo la maziwa makuu.
"Nishani hizi tofauti nilizowavalisha leo kwa niaba ya Rais, tambueni ni heshima aliyoitoa kwa majeshi yetu tukitimiza miaka 60 ya Muungano wetu, mkaongeze bidii ya kazi na kuwa mfano kwa wengine,"Dkt. Anna Makakala, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji.
Kamishna Jenerali huyo amewavisha nishani tofauti kwa Maafisa Wakaguzi na askari wa Uhamiaji kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera, Simiyu, Geita, Kigoma, Mara, Tabora na Shinyanga.
Nishani walizovalishwa Maafisa hao ni ya Muungano,Utumishi uliotukuka,Utumishi wa muda mrefu na tabia njema na utumishi wa muda mrefu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.