RC MTANDA AWATAKA MGAMBO WA JIJI KUZINGATIA SHERIA, TARATIBU NA KANUNI WAKATI WA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka askari wa Jeshi la Akiba (Mgambo) wa Jiji la Mwanza kuzingatia na kutekeleza sheria, taratibu na kanuni katika zoezi la ukamataji wa wafanyabiashara wanaokiuka sheria na kanuni zilizowekwa katika maeneo rasmi ya kufanyia biashara na kupanga biashara zao barabarani.
“Askari Mgambo anayo amri ya ukamataji na anapokamata anatakiwa azingatie sheria lakini anayekamatwa naye anatakiwa kutii sheria bila shuruti”, amesema Mtanda.
Akizungumza leo Julai 5, 2024 kwenye kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mtanda ameutaka uongozi wa Jiji la Mwanza chini ya Mkurugenzi wake kuharakisha ujenzi wa masoko sahihi ili kuepusha migogoro inayojitokeza.
“Ili kupunguza adha ya wafanyabiashara kuzurura na kupanga bidhaa kwenye barabara ni vizuri masoko haya yakamilishwe kwa wakati ili wapate maeneo mazuri yakufanya biashara” Mkuu wa Mkoa.
Naye, msimamizi wa askari wa Jiji Mwanza SSP Philoteus Ngosingosi amesema Juni 20, 2024 alikabidhiwa rasmi na Uongozi wa Jiji kuendesha shughuli ya kuelimisha, kukamata na kuwafikisha mahakamani na kutoa adhabu wafanyabiashara ambao hawataki kufata sheria na kanuni zilizowekwa.
Mkoa wa Mwanza unachangia asilimia 7.1 katika pato la Taifa hivyo kulipa kodi ni wajibu na sheria ili kuleta maendeleo ya nchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.