RC MTANDA AWATAKA VIJANA KUTUMIA SIMU JANJA KUJILETEA MABADILIKO YA KIUCHUMI
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka Vijana wa Mkoa wa Mwanza kutumia simu janja kwa matumizi sahihi ili waweze kujiletee manufaa katika kujikwamua na umaskini na kuacha kutumia muda mwingi katika mitandao kwa kutukana watu na kuwachafua.
Mhe. Mtanda ametoa wito huo leo Novemba 29, 2024 wakati alipokuwa akizindua dukala simu la Zahor Matelephone lililopo Mtaa wa Lumumba Jijini Mwanza, Mhe. Mtanda amesema simu janja zinaweza kutumiwa vizuri na kuondoa umaskini kupitia biashara mtandao.
"Wako wananchi wa Vijijini wanaweza kuangalia bei za mazao kwenye minada kupitia simu za Zahor Matelephone ambazo zinauzwa elfu 70, lakini wavuvi wanaweza kuangalia hali ya hewa kupitia smartphone ndipo wakaingia ziwani".
Sasa kushinda kwenye mtandao asubuhi hadi jioni, unaangalia habari ambazo hazina tija ni kupoteza muda na duniani hakuna kitu cha thamani kama muda, wakati ni ukuta, tukiutumia vibaya tunajiondoa katika ule mzunguko wa kujitoa katika hatua moja kwenda nyingine ya kimaisha. Ameongeza Mhe. Mtanda.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesema Serikali itaendelea kumaliza changamoto hatua hatua ambapo kwa siku kadhaa zijazo soko la kimkakati la Mjini Kati litafunguliwa rasmi ambapo wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati watapatiwa sehemu ya kujipatia riziki.
Sambamba na hayo Mhe. Mtanda amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Mwanza waliopata nafasi ya kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa amani, na amewataka wananchi kuendelea kuchapa kazi ili waweze kujipatia riziki kwa kuwa uchaguzi sasa umekwisha.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.