RC MTANDA AWATAKA WANA ILEMELA KUTUMIA VYEMA TAREHE ZA KUJIANDIKISHA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka wananchi wa Wilaya ya Ilemela kuhakikisha wanatumia vilivyo terehe 11 - 20 Oktoba 2024 kwa kujiandikisha katika daftari la uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji .
Mhe. Mtanda amesema wakati watu wa makundi mengine wako na agenda zao za kuzurura amewataka wana Ilemela kutumia fursa hiyo katika kujiandikisha kwa wingi ili wakawachague viongozi ambao ni sahihi kwa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji.
Mkuu huyo wa Mkoa ameyasema hayo mapema leo Septemba 23, 2024 wakati akizungumza na Viongozi na wananchi zaidi ya elfu tatu waliojitokeza katika mkutano maalumu wa kujadili namna ya ushiriki wa kilele cha mbio za mwenge utakaofanyika Kitaifa katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mkoani Mwanza.
"Miaka 60 siyo mchezo, mwenge una mri mkubwa kuliko umri wa watu wengi hapa, sasa sio mchezo miaka 60 mwenge ukiwa unawaka katika nchi yetu hivyo kushirkki katika hafla hiyo ni neema kubwa sana" Amesema Mhe. Mtanda.
Naye Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobass Katambi (MB), amesema mwenge unaleta kumbukizi ya tulikotoka, kumbukizi ya viongozi wetu waliotangulia mbele za haki, lakini pia ni heshima kubwa kwa mwenge kufika Mkoani Mwanza huku tukiwa tunaelekea kwenye uchaguzi kwa kuwa ni hamasa pia.
Kadhalika amewataka wananchi hao kwenda kuhamasisha wananchi wengine kushiriki katika kilele cha mbio za mwenge pale CCM Kirumba na kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt. Samia kwa yale maendeleo makubwa aliyoyafanya katika Mkoa wa Mwanza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.