RC MTANDA AWATAKA WATUMISHI KUCHAPA KAZI, KUACHA UBADHIRIFU FEDHA ZA UMMA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Juni 10, 2024 amezungumza na watumishi wa Halmashauri na taasisi mbalimbali wilayani Sengerema na ametumia wasaa huo kuwataka kuchapa kazi kwa bidii na kutofanya ubadhirifu wa fedha za umma.
Amesema siku za nyuma Halmashauri hiyo ilikua na doa la kutosimamia vema miradi ya maendeleo na kukiuka taratibu za utumishi wa umma na kupelekea kupata hadi Hati zenye mashaka kutoka kwenye ripoti za ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali.
"Ni lazima tuchape kazi kwa moyo na si kwa sababu tunalipwa mshahara bali tufanye kazi kama Ibada kwa kuwatumikia wananchi kwa moyo wa upendo na tutapata thawabu kwa Mwenyezi Mungu, hivyo tuwe na huruma tunapowapokea wananchi kwenye ofisi zetu." Mkuu wa Mkoa.
Aidha, ametaka kuwepo kwa nidhamu kazini kwa kuwahi kufika, kufanya majukumu na kutekeleza maelekezo ya viongozi na kwamba mtumishi akifanya vinginevyo basi atakua mtovu wa nidhamu kwani malengo ambayo Serikali inategema yatimizwe hayatofikiwa.
Hali kadhalika, amesisitiza suala la ushirikiano na uhusiano wa kikazi baina ya ofisi na ofisi lakini pia watumishi ndani ya ofisi ili kuwa na maelewano mazuri na kuhakikisha wanafanya kazi kwa pamoja ili kujenga taswira njema kwa wananchi wanaohudumiwa.
"Kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2023/24 wilaya iliidhinishiwa kukusanya kiasi cha Tshs. 6,175,910,555 na hadi kufikia Mei mwaka huu wilaya imefanikiwa kukusanya Tshs. 695, 335,706 sawa na asilimia 98.69 hata hivyo mapato ya Halmashauri zote yamekua yakiongezeka." Mhe. Senyi Ngaga, Mkuu wa Wilaya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.