RC MTANDA AZINDUA OFISI ZA PPRA KANDA YA ZIWA, AMPONGEZA RAIS SAMIA KUSOGEZA HUDUMA KWA WADAU
Leo Juni 11, 2024 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amezindua Ofisi ya Kanda ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma zilizopo mtaa wa Mkoani kwenye jengo la zamani la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Akizungumza kwenye hafla hiyo fupi Mhe. Mtanda amesema uwepo wa Ofisi hiyo ni ishara ya Kujali na uhodari wa Rais Samia kwenye kuboresha ofisi za umma nchini hivyo ametumia wasaa huo kumshukuru kwa kusogeza huduma kwa wadau wa ununuzi nchini.
"Tunaamini watatoa huduma bora kwa taasisi nunuzi kwa kuzingatia matumizi sahihi ya mfumo ili kurahisisha huduma na kuwa na thamani ya fedha za umma kwenye ununuzi", amesema Mkuu wa Mkoa wakati akiwasihi PPRA kutoa huduma bora.
Katibu Tawala Mkoa, Balandya Elikana amesema mifumo ya ununuzi wa umma ya Elektroniki ina faida ya kuweka uwazi wa kuonesha huduma au bidhaa kwa wazabuni na inasaidia kupunguza upendeleo na rushwa na kupatikana kwa thamani ya fedha kwenye huduma au bidhaa iliyotolewa.
Mhandisi Juma Mkobya, Meneja PPRA kanda ya ziwa amesema ufunguzi wa kanda hiyo tangu machi 20, 2024 ili kuhudumia mikoa ya Mwanza, Simiyu, Kagera na Mara umelenga kusogeza huduma kwa wadau wa ununuzi walio kenye ukanda huo pamoja na kutoa mafunzo kwa wazabuni.
"Lengo kuu la ufunguzi wa kanda hizo umelenga kusogeza huduma kwa wadau na kwamba katika kuhakikisha wanawaunganisha watumishi walio kwenye mamlaka za Serikali za mitaa pamoja na taasisi zingine tayari tumetembelea halmashauri zote pamoja na taasisi kuwapa mafunzo." Mkobya.
Aidha, Mhandisi Mkobya ametumia wasaa huo kuwataka taasisi kutoa mafunzo kwa wadau na wazabuni ili wapate uelewa wa kutosha ili kuondokana na changamoto za utumizi wa mfumo huo kutokana na ugeni kwenye masuala ya ununuzi na ugavi kwani miaka ya nyuma ambapo ulikua hautumiki mfumo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.