• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC MTANDA AZINDUA WIKI YA MAZIWA KITAIFA, AWATAKA WANANCHI KUNYWA MAZIWA SALAMA

Posted on: May 29th, 2024

RC MTANDA AZINDUA WIKI YA MAZIWA KITAIFA, AWATAKA WANANCHI KUNYWA MAZIWA SALAMA.


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka wananchi wa Mkoa huo na kote nchini kunywa Maziwa yaliyosindikwa ili kujihakikishia usalama na ubora wa bidhaa wanayotumia kwa ajili ya kujenga jamii yenye afya.

Mhe. Mtanda ametoa wito huo leo Mei 29, 2024 wakati akizindua Maadhimisho ya 27 ya wiki ya Maziwa Kitaifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Furahisha Ilemela - Mwanza huku kilele chake kikitarajiwa kuwa tarehe 01 Juni, 2024.

Amesema, kwa wastani mtanzania anakunywa lita 67.5 kwa mwaka wakati malengo ya kidunia ni kunywa lita 200 kwa mwaka na kwa Mwanza kuna ng'ombe 16,223 ambapo ni wastani wa lita elfu 85 kwa siku ambapo kwa ujumla ni kiasi kidogo.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kutumia maziwa yaliyosindikwa na wazawa ndani ya mkoa ili kukuza uchumi wa wale wote wanaojihusisha na uzalishaji ndani ya Mkoa wa Mwanza na kujijengea utamaduni wa kunywa glasi moja ya maziwa kwa siku.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri Prof. Zacharia Masanyiwa ametumia jukwaa hilo kuwaalika wafugaji kwenye viwanja hivyo ili kujifunza usindikaji na kuboresha mnyororo wa thamani kwani kwa sasa sekta hiyo ina mchango mdogo kwenye Pato la Taifa yaani kwa asilimia 2 tu.

Msajili wa Bodi ya Maziwa nchini Prof. George Msalya amesmea kuwa Maziwa ni mlo kamili unaojitosheleza kwa kuwa na virutubisho vyote kama vile Madini na Vitamini na kwamba wananchi wana kila sababu kuyanywa.

Aidha, amebainisha mchango wa sekta hiyo kwenye ajira kwani kaya milioni 2.2 nchini zinajihusisha na uzalishaji na kuajiri watu na kwamba wadau zaidi ya Elfu 7 wanajihusisha kwenye mnyororo wa thamani.

Maadhimisho hayo ya Kitaifa kwa Mwaka 2024 yanaenda sambamba na kauli mbiu isemayo; 'Kunywa Maziwa Salama kwa Afya Bora na Uchumi Endelevu.'

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.