RC MTANDA AZUNGUMZIA MIKAKATI MIZITO YA PAMBA JIJI FC
Mashabiki wa soka Mkoani Mwanza wameombwa kuwa na subira wakati timu yao ya Pamba Jiji FC itakayoshiriki ligi kuu msimu ujao ikiwa inaendelea kuwekewa mikakati kamambe ikiwemo dawati jipya la ufundi lenye mchanganyiko wa wataalamu mahiri wa nje na ndani ya nchi, litalotangazwa hivi karibuni, wachezaji wapya na kambi ya maandalizi ya timu hiyo.
Akizungumza mapema leo asubuhi kwenye kipindi cha Morning Trumpet kinachorushwa Mubashara na chaneli ya UTV ya Azam TV, Mtanda amebainisha wamejipanga kumpata kocha mahiri ambaye atasimamia zoezi la kuwapata wachezaji bora na kuingia mapema kambini kujiwinda na kishindo cha ligi kuu.
"Tunahitaji muda wa wiki 5 wa kujiandaa na ligi kuu, tunatambua ushindani uliopo na hasa ubora wa timu zote shiriki, hivyo nasi ni lazima tuwe bora zaidi", amesisitiza mkuu huyo wa Mkoa.
Mtanda ambaye ni mkereketwa wa mchezo wa soka amesema wameweka mpango maalum wa kuinua soka Mkoani humo kwa kuwapa nafasi zaidi wachezaji wanaotokea Mwanza naeneo la Kanda ya ziwa watakaochanganyika na wageni.
Pamba Jiji FC maarufu kama wana TP Lindanda wamefuzu kucheza ligi kuu ya NBC msimu ujao pamoja na Kengold kutoka Mbeya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.