RC MTANDA MBIONI KUWAKUTANISHA MAAFISA USAFIRISHAJI NA TAASISI ZA KIFEDHA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewahakikishia kuwakutanisha na taasisi za fedha mara watakapokuwa tayari Maafisa usafirishaji wa Bajaj na Bodaboda baada ya kuweka bayana changamoto za kuendesha shughuli zao na wamiliki wa vyombo wanavyotumia.
Akiwa katika zoezi la kuzungumza na makundi mbalimbali leo Septemba 25,2024 kwenye viwanja vya Furahisha ikiwa zamu ya kundi hilo, Mhe. Mtanda amebainisha lengo la Serikali ya awamu ya sita ni kuona wanaojiajiri wanafanya shughuli zao kwa tija.
Amesema Serikali inatambua mchango wa maafisa usafirishaji hao katika kujenga uchumi wa nchi hivyo atahakikisha changamoto zinazowakabili zinafikishwa kwenye Taasisi za kifedha ili ufumbuzi wa kuwakwamua upatikane.
"Sasa mjipange na kuniambia lini mtakuwa tayari ili niwaitishie mkutano na Taasisi za fedha ili mzungumze yote ya yanayowakwamisha",Mkuu wa Mkoa.
"Ndugu yetu Mkuu wa Mkoa awali ya yote tumefarijika kuja kuzungumza nasi,wengi tumeingia mikataba ya kuendesha vyombo hivi na wamiliki ili baadaye viwe chini yetu, lakini tunajikuta tukilipa fedha nyingi kuliko Ile bei halisi na wengine wakishindwa na kuingia katika migogoro,"Zakayo Mashamba,Katibu chama cha Maafisa usafirishaji.
Katika mkutano huo Mkuu huyo wa Mkoa amewakumbusha umuhimu wa kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba 27 mwaka huu na kujiandikisha pia kwenye daftari la kudumu la kupiga kura kuanzia Oktoba 11 hadi 20.
Aidha amewataka kuendelea kuilinda na kuitetea amani yetu kwa kutokubali kutumika kisiasa na badala yake kuchapa kazi na kushirikiana na vyombo vya usalama pindi waonapo dalili au mtu yoyote anaetaka kuivunja amani yetu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.