Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe,Mhandisi Robert Gabriel amezitaka Halmashauri zote Mkoani humo kuisimamia na kuitekeleza kwa Weledi Miradi yote ya Elimu na Afya.
Mhe.Mhandisi Gabriel ameyasema hayo katika Kikao cha Mpango Kazi kilichowashirikisha viongozi wote kutoka Halmashauri za Mkoani Mwanza na wadau mbalimbali wa Elimu na Afya Mkoani humo.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema Wananchi hawana muda wa kusubiri Maendeleo katika maeneo yao zaidi ya kuwaharakishia ili kazi za kujenga Taifa ziendelee.
"Kuna Miradi ya Afya inaendelea kufanyika na baadhi ya Wilaya tayari zimenikabidhi,lakini bado kuna changamoto za hapa na pale ambazo ni lazima tushikamane kuzitatua" amesema Mkuu huyo wa Mkoa.
Mhandisi Gabriel amesema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inasukuma Miradi ya Maendeleo kona zote za nchi hii,lengo likiwa ni kulijenga Taifa imara katika Sekta zote ikiwemo Elimu na Afya.
Katika kikao hicho cha mpango kazi kilimpongeza na kumkabidhi Tuzo Mkuu huyo wa Mkoa wa Mwanza pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa huo,Ngusa Samike kutokana na usimamizi na ufuatiliaji mzuri wa Miradi mbalimbali inayotekelezwa Mkoani humo.
Kikao cha mpango kazi kinafanyika kwa lengo la kuhimiza na kuangalia sehemu zenye changamoto na kuzitatua katka Miradi mbalimbali inayofanyika Mkoani Mwanza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.