Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mhe Mhandisi Robert Gabriel amewahimiza Wakazi wa Mkoa huo kutumia kikamilifu Wiki ya Huduma za Maabara zitakazo fanyika viwanja vya Furahisha kuanzia Mei 2 hadi 6 mwaka huu, ili waelimike na kupata ufumbuzi wa Maradhi mbalimbali yanayowanyemelea.
Akizungumza katika mkutano na Vyombo vya Habari Mkoani Mwanza,Mkuu huyo wa Mkoa amesema bado Wananchi wengi wanasumbuliwa na ufahamu kuhusu Maabara na kujikuta wanapatwa na Maradhi kutokana na kutofahamu kazi sahihi za Maabara.
"Wananchi hii haijawahi kutokea nawaombeni mchangamkie fursa hii na pia tuwachangie Damu ndugu zetu waliopo Hospitali wenye kuhitaji huduma hiyo" amesisitiza Mhandisi Gabriel.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dktr Thomas Rutachunzibwa amesema Wiki ya Huduma ya Maabara inawakutanisha Wananchi na Wataalamu wa huduma hizo,hivyo wana imani ya kupata matokeo chanya.
"Kumekuwepo na ongezeko la Maradhi ya Saratani hasa Mikoa ya Kanda ya Ziwa,Wataalamu wetu wa Utafiti wapo kazini ili kuja na jibu sahihi kiini cha tatizo hili na idadi halisi,niwatake Wakazi wa maeneo haya ya Kanda ya Ziwa kuwa na subira" amesema Dktr Rutachunzibwa.
Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Maabara hufanyika ulimwenguni kote kila mwaka mwishoni mwa Aprili,kauli mbiu ya mwaka huu inasema "Vipimo vya Maabara za Afya ndiyo msingi wa matibabu bora" Kazi iendelee.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.