REO MWANZA AFANYA TATHIMINI YA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE NA KUTOA MAAGIZO KWA SHULE ZILIZOFANYA VIBAYA
Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza Martin Nkwabi amefanya kikao na walimu wakuu wa shule zote za Sekondari za mkoani humo ambazo zimefanya vibaya kwenye matokeo ya kidato cha nne mwaka 2023-2024
Amesema hayo leo Februari 06, 2024 katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa ambapo amekutana na walimu wakuu wote wa shule za Sekondari zilizofanya vibaya katika matokeo ya Kidato cha nne Mwaka 2023-2024 ambapo ni tathimini ya kimkakati ya kila mwaka kwa lengo la kutokomeza ufaulu usiokidhi viwango na kupandisha ufaulu mkoani humo.
“Mwaka jana tulikuwa na shule 53 zilizokuwa na ufaulu mbaya na kati ya hizo ni shule 21 tu ndo ambazo wamefanikiwa kupandisha ufaulu wao mwaka huu, hao wengine wameporomoka sana kulinganisha na matokeao ya zamani na shule hizi zinatoka katika halmashauri ya ukerewe, Jiji la Mwanza Misungwi hazijafanikiwa kupandisha ufaulu kabisa na kukidhi viwango vya ufaulu”, amesema Nkwabi.
Lakini pia amewapongeza sana walimu wa taaluma kwa jitihada zao za kuhakikisha shule zinafanya vizuri katika matokeo, pia ametaka walimu wakuu wa shule huu mwaka kuwa wa mwisho kwa matokeo mabovu katika shule zao.
Nae Afisa Taaluma Mkoa wa Mwanza Aisa Rupia ametoa orodha ya shule zilizopandisha ufaulu na ambazo hazijapindisha ufaulu katika mkoa huo, lakini amezitaka shule zingine kuiga mfano kwenye shule zilizofanya vizuri na kufuta sifuri na rai yake ni kutaka shule zote zipate matokeo chanya huku akihamasisha uwajibikaji na kujitoa mashuleni.
“Tunazipongeza kwa dhati shule zilizofuta daraja sifuri rai shule ziandae mikakati ya kufuta sifuri katika mkoa wa Mwanza wanafunzi wajengewe uwezo wa kufanya vizuri zaidi kitaaluma,”amesema Afisa Taaluma
Huo ni muendelezo wa kuleta matokeo chanya ya kielimu katika mkoa wa Mwanza kwenye shule za Sekondari, tathimini hizo hufanyika kila mwaka kwa dhumuni la kuboresha kupandisha ufaulu na kutokomeza sifuri.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.