Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Mhe,Hassan Masala amewataka Walimu na Viongozi wa Skauti wanaoendelea kupata Mafunzo ya kutokomeza rushwa Mkoani humo kutumia nafasi hiyo vyema kuelimisha Jamii ili kujenga vizazi vyenye weledi wa kulijenga Taifa
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa kauli hiyo kwa niaba yake na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilemela,Said Kitinga wakati akifunga Mafunzo ya kutokomeza rushwa kwa Walimu walezi na Viongozi wa Skauti Wilayani humo amewakumbusha Washiriki hao rushwa ni adui wa haki hivyo haina budi kupingwa kwa nguvu zote.
Amesema kwa kutambua mchango wa Walimu katika uelimishaji Jamii huku Vijana nao wakiwa ndiyo nguvu kazi ya Taifa,Makundi hayo yataleta matokeo chanya kwa Jamii baada ya kupata mafunzo hayo.
Kamanda wa Takukuru Wilaya ya Ilemela,Nobert Ndika amesema bado Jamii inahitaji elimu ya mara kwa mara kuhusu aina za rushwa na madhara yake.
Mkuu wa Dawati la Uelimishaji kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa Wilayani Ilemela,Doreen Ntongani amesema Jamii ikipata uelewa wa kutosha kuhusiana na ubaya wa rushwa ni dhahiri nchi itakuwa na watu wenye kuheshimu majukumu yao bila kuwanyanyasa wengine, huku baadhi ya washiriki wakiipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe Rai's Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kutaka kuwa na Jamii yenye kuishi kistaarabu
Mafunzo hayo ya kutokomeza rushwa yanayofanyika nchi nzima,yalizinduliwa Kitaifa Mkoani Dodoma mwaka Jana na Mhe Rai's Samia Suluhu Hassan na kuendelea ngazi ya Mkoa na Wilaya nchini kote.
Taasisi ya kuzuia na Kupambana na rushwa, Takukuru pamoja na Chama cha Skauti Taifa wamepewa jukumu hilo la kutoa Mafunzo hayo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.