Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella ameahidi kuunda tume ili kuchunguza suala la utoro linaloikabili shule ya sekondari Maisome wilayani Sengerema baada ya kuelezwa kuwa ni wanafunzi 29 tu kati ya 80 waliohitimu kidato cha nne mwaka jana.
Mhe. Mongella amechukua hatua hiyo baada ya kupokea mradi wa jengo la utawala na samani ya shule ya sekondari Maisome uliotekelezwa na shirika la hifadhi la taifa ( TANAPA) ambapo amewataka wazazi, watendaji na wadau wa elimu kuchukua hatua za haraka kujenga mabweni kudhibiti suala la utoro shuleni hapo.
Mhe. Mongella ameongeza kuwa licha ya elimu bure bado wanafunzi wengi wameendelea kukosa elimu kutokana na uduni wa kipato na mimba za utotoni ambazo chanzo kikuu inadaiwa ni wanafunzi kulazimika kutembea umbali mrefu kila siku kusaka elimu na katikati ya njia hukumbana na vishawishi vingi.
Kutokana na kiwango kikubwa cha utoro Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella ameahidi kuchunguza suala hilo.
Baadhi wanaamini ujenzi wa mabweni unaonekana kuwa suluhisho la tatizo la utoro na mimba za utotoni.
Mbali na kuzindua jengo la utawala la shule ya sekondari Maisome Mhe. Momgella pia ametembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa sekondari ya Kasisa, na ujenzi wa hospitali ya Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.