SEKTA YA MADINI INAENDELEA KUKUA KWA KASI NCHINI : WAZIRI MAVUNDE
Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema Sekta hiyo inazidi kukua ambapo 2022/23 Mauzo ya bidhaa za Madini nje ya nchi yalifikia 56% huku Mzunguko wa fedha ukichangia zaidi ya Trilioni 1.6 na zaidi ya Bilioni 678 zikikusanywa kama Maduhuli ya serikali zinazotokana na vyanzo mbalimbali vya mapato kwa zaidi ya Trilioni 2 ambayo ni 15% ya pato lote.
Mhe. Mavunde amebainisha hayo mapema leo tarehe 05 Januari, 2024 kwenye Ukumbi wa Rock City Mkoani Mwanza wakati akizungumza na watoa huduma kwa wamiliki wa Leseni za Madini kwenye Mkutano uliowakutanisha wadau ili kujadili namna bora ya kuboresha sekta hiyo ili washiriki kwenye Uchimbaji waongezeke.
"Hadi sasa tumefanya utafiti kwa 16% na lengo letu kubwa ni kubaini madini tuliyonayo na kuweza kujipanga ili kusaidia wananchi kuacha kufanya uchimbaji kwa kuhisi na hadi kufikia 2030 wananchi watakua wanajua hapa kuna nini kwa taarifa sahihi kutoka wizara ya Madini." Waziri Mavunde.
Vilevile, amebainisha kuwa wizara ya Madini ipo tayari kufanya maboresho ya kisheria ili kutoa fursa zaidi kwa washiriki kuweza kujihusisha na uchimbaji wa Madini nchini huku akitoa wito kwa taasisi za kifedha kuendelea kuwezesha mitaji ili watanzania wengi washiriki kwenye kuchimba na kuchangia rasilimali kwenye utoaji huduma kigodini.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla ameipongeza Wizara ya Madini kwa kufanya Utafiti wa kubaini ni eneo gani lina Madini ya aina gani na kwa kiasi gani kwani litasaidia kupunguza gharama za uendeshaji kwenye sekta hiyo nchini.
"Hakika Waziri Mavunde unafanya kazi nzuri kwa manufaa ya watanzania, ulipokua Naibu kwenye Kilimo ulifanya tafiti kuhusiana na Afya ya Udongo na huku kwenye Madini umekujq na jambo zuri la kubaini ni wapi kuna madini, ya aina gani na kwa kiasi gani, hapa utasaidia." Makalla.
Aidha, Mhe. Makalla amebainisha kuwa uwanja wa ndege wa Mwanza upo kwenye maboresho makubwa kuanza kuhudumia wasafiri na wasafurishaji wa Mizigo hivyo wadau wa sekta ya Madini watapata fursa ya kusafirisha bidhaa hizo kwenda nje ya nchi kwa ufanisi.
"Kutakua na Mgodi Mkubwa wa Madini ya Dhahabu wilayani Sengerema (Nyanzaga) ambao utashika nafasi ya Pili nchini ambao upo kwenye hatua mwisho kuanza kazi, nawaomba wanaMwanza mjiandae kunufaika na fursa." Makalla.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.