SERIKALI IMEENDELEA KUKUSANYA MAONI YA MAREKEBISHO SERA YA MAMBO YA NJE YA MWAKA 2001:NAIBU WAZIRI MBAROUK
Serikali imeendelea kukusanya kukusanya maoni ya Watanzania kuhusu marekebisho ya sera ya mambo ya Nje iliyotungwa mwaka 2001 na kuanza kutumika 2004 ambayo imekuwa haitoi fursa pana katika majukwaa ya kimataifa na ndani ya nchi.
Akizungumza kuhusu sera hiyo leo Aprili,19 2024 kwenye ukumbi wa mikutano,Gold Crest Naibu Waziri wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe:Mbarouk Nassoro Mbarouk wakati wa kongamano la tano Jijini Mwanza amebainisha maoni hayo wanaamini yatakuwa na mchango mkubwa wa kuleta mageuzi ya kimaendeleo.
“Tanzania kama yalivyo Maataifa mengine inakabiliwa na fursa na changamoto katika ushiriki kwenye majukwaa ya kanda na kimataifa hivyo kuwa na sera madhubuti ni muhimu ili kutumia fursa zinazotokana na ushiriki wa nchi zetu kwenye majukwaa hayo ikiwa pamoja na kukubaliana vyema na changamoto zinazojitokeza”
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe:Hassan Masala aliyekaimu nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, amesema Mkoa wa Mwanza ni kitovu cha biashara kwakuwa imezungukwa na nchi jirani kama Rwanda na Burundi vivyo ni muhimu kwa mkoa huo kutoa maoni na mapendekezo kuhusu marekebisho ya sera mpya ya mambo ya nje ya mwaka 2001.
“Tuna mkoa wa kimkakati ambao nchi za maziwa makuu unautegemea katika shughuli za kiuchumi zikiwemo za uvuvi,madini na usafirishaji" Mkuu wa Wilaya
"Huu uraia pacha binafsi sioni kama una mashiko japo nasikia ukipigiwa sana debe,tujivunie utaifa wetu,mtu akienda nje basi aamue abaki na utaifa wake au aombe huko alipo",Masala Kulangwa,Mwenyekiti Baraza la Wazee.
"Nashauri huu uteuzi wa mabalozi uanzie ngazi ya chini kwa wananchi kushirikishwa ili kuwepo na uwazi na kumpata mtu sahihi atakaye kwenda kuiwakilisha nchi yetu," Irine Joseph,mwana zuoni,SAUT
"Vyombo vya habari nashauri viongezewe uwanda mpana wa kufanya kazi zake hasa kutokana na utanda wazi uliopo sasa,naipongeza Serikali kwa uamuzi huu wa marekebisho haya",Issa Hussein,mtoa maoni.
Baadhi ya wadau walioshiriki kutoa maoni ni wanasiasa,viongozi wa Baraza la wazee ,wakuu wa Taasisi za umma,wana zuoni, na wahadhiri.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.