SERIKALI ITAENDELEA KUTHAMINI MCHANGO WA WANASAYANSI NCHINI - DKT. BITEKO
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na kuwajengea mazingira mazuri wanasayansi nchini ili kuenzi mchango wao katika kuimarisha sekta ya afya.
Dkt. Biteko ametoa wito huo leo Novemba 13, 2024 wakati akifungua Kongamano la Kimataifa la Sayansi lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi (CUHAS) katika hoteli ya Malaika Ilemela Mwanza.
Amesema wanasayansi wana mchango mkubwa katika kukabili majanga ya kiafya mathalani maradhi ya mlipuko kupitia tafiti zao wanazofanya ambazo zinatoa majibu ya chanzo na namna ya kukabiliana na maradhi fulani kupitia machapisho wanayotoa.
Aidha, amewapongeza Chuo Kikuu cha Sayansi Bugando kwa kutoa zaidi ya machapisho 150 ya kisayansi yanayotoa mchango mkubwa kwenye upangaji wa sera nchini na kwa kipekee Prof. Steven Mshana ambaye ameibuka kuwa mwanasayansi bora wa mwaka 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema wananchi wa Mkoa huo wanaishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania kwa kuupatia Mkoa huo fedha zaidi ya Tshs. Trilioni 6 kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Vilevile, amebainisha kuwa wananchi wa Mkoa huo wanajivunia uwepo wa Ziwa Victoria ambalo wanalitumia kuwainua kiuchumi katika shughuli za uvuvi na kwamba wananchi wake wana afya njema wanaendelea kuchangia pato la Taifa kwa zaidi ya asilimia 7.2.
Kongamano hilo la 14 lililoandaliwa na hospitali ya kanda ya rufaa Bugando na chuo kikuu cha sayansi kimewakutanisha zaidi ya wataalamu 450 kutoka ndani na nje ya nchi wanaokutana kujadili mustakabali wa magonjwa na namna ya kuyakabili.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.