Kamati ya lishe Mkoa wa Mwanza imefanya kikao chake cha robo ya kwanza ya mwaka 2018/2019 pamoja na kikao cha tatu cha kamati tendaji ya 'program ya right start initiative' kilichofanyika katika ukumbi wa Mipa Hoteli Jijini Mwanza.
Kikao hicho kimejadili taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri robo ya nne 2018/19 pamoja na taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe katika sekta mbalibali ikiwa ni pamoja na sekta ya kilimo na wadau wa lishe kama vile Amref Health Africa.
Akiongea katika kikao hicho Mwenyekiti wa Kikao ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bwana Christopher Kadio amesema Makamu wa Rais amekuwa akifatilia kwa ukaribu swala la Lishe na kuomba taarifa za mara kwa mara.
"Maagizo ya Serikali tulipe uzito swala la lishe,hivyo baada ya miezi 3 Halmashauri zote ambazo hazina vitengo vya lishe zihakikishe zinaanzisha,"alisema Kadio.
Aidha,Kadio ameongeza kuwa hata katika kikao vya menejimenti kuwe na agenda ya lishe kwani kwa kufanya hivyo swala la kuondoa utapiamulo litapewa uzito ikiwa ni pamoja na kutenga bajeti ya kutoa huduma katika vituo mbalimbali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.