Serikali imetoa pongezi kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Sekou Toure kwa uboreshaji wa huduma na ameagiza hali hiyo iwe endelevu kwa faida ya Wananchi.
Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollei leo amefanya ziara fupi Hospitalini hapo Kwa kutembelea jengo jipya la huduma za Mama na Mtoto na kufanya kikao na Watumishi wake.
Amesema kumekuwa na mabadiliko chanya siku hadi siku wakati Serikali ikiendelea kufanya maboresho kwenye kila sehemu yenye uhitaji.
"Nimekuwa nikiifuatilia Hospitali hii nasema wazi kabisa mmebadilika na hongereni sana, hali hii inamtia moyo hata Rais wetu Mhe Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa mstari wa mbele kupigania Maendeleo ya Taifa letu" amesema Mhe Mollel.
Aidha Mhe Mollel amezipongeza asasi zisizo za Kiserikali zinazofanya kazi chini ya Wizara ya Afya ambazo zimekuwa chachu ya Maendeleo katika Sekta ya Afya nchini.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt Thomas Rutachunzibwa amesema wadau wa Maendeleo Mkoani humo wamekuwa nguzo muhimu katika Miradi ya Afya hasa sehemu za vijijini na kufanya huduma hiyo kuwa rahisi kwa kutoa elimu na tiba.
Mkurugenzi kutoka Shirika la Americares wanaojihusisha na Mradi wa Uzazi Staha, John Fulli amesema kwa kutambua umuhimu wa Sekta ya Afya wataendelea kushirikiana na Serikali ili kufikia malengo yaliyokusidiwa.
Naibu Waziri Dktr Godwin Mollel yupo Mkoani Mwanza kwa ziara ya kukagua Miradi ya Sekta ya Afya na kuzungumza na Watumishi wake.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.