Jumla ya Shs Trilioni 1.15 zimetengwa na Serikali mwaka huu Kwa ajili ya kuboresha Elimu ya awali na Msingi nchini huku kipaumbele kikiwekwa cha kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani na uimarisharishaji wa miundombinu Shuleni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Angella Kairuki amesema hayo leo Mkoani Mwanza wakati wa kufunga kikao kazi cha Tathmini ya uboreshaji elimu mwaka 2022-23 na mkakati wa mwaka huu wa mabadiliko kwenye Sekta hiyo kilichowakutanisha walimu wa Msingi na Sekondari, na Maafisa Elimu wa ngazi zote Mkoani humo,amesema mpango huo utaondoa adha yote ya msongamano wa wanafunzi waliozidi idadi ya 60 darasani na kujengwa madarasa mengine.
"Huu ni mpango wa miaka mitano ambapo Shule zote zenye wanafunzi wa zaidi ya 1500 zitajengwa Shule nyingine ambapo jumla ya Shs bilioni 250.6 zitatumika kujenga madarasa 9000 nchi nzima"amesema Mhe Waziri.
Ameongeza kuwa kata 3900 zilizopo nchini zitanufaika na kupata shule moja za Sekondari kutokana na fedha nyingine iliyotengwa shs Trilioni 1.2 na kusisitiza Serikali ya awamu ya Sita imedhamiria kwa vitendo kuiboresha sekta hiyo ili watoto wote wapate elimu bora na wasome katika mazingira rafiki.
" Mhe Rais ameonesha namna alivyopania kumletea maendeleo mwananchi kwa kutoa kiwango kikubwa cha fedha,wajibu wetu sasa sisi walimu na tuliopewa dhamana ya uongozi ni kumuonesha kiongozi wetu wa nchi matokeo chanya kwenye elimu ukiwemo ufaulu mzuri Msingi na Sekondari na mwamko wa juu wa watoto kuandikishwa shule".Amehimiza Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Elimu,Dkt.Charles Msonde.
"Mkoa wa Mwanza tumeendelea na mkakati wa kuboresha Elimu na kufanikisha kukamilisha ujenzi wa madarasa kwa wakati kwenye Wilaya zote japo changamoto iliyopo ni uhitaji wa jumla ya walimu 9442. Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Hassan Masala.
"Tumepokea na tutaifanyia kazi miongozo yote iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Dkt.Charles Msonde inayotaka kuja na matokeo chanya katika Maendeleo ya Sekta hiyo Mkoani kwetu".Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza,Martine Nkwabi
Kikao kazi hicho pia kimewashirikisha Wakuu wote wa Wilaya, na Wakurugenzi wa Halmashauri kutoka Mkoani Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.