Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amekabidhi vitabu 38,891 vya darasa la nne kwa shule zote za msingi Wilayani Ukerewe.
Akiongea katika makabidhiano hayo Mhe.Mongella amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI imeendelea kutilia mkazo juu ya elimu na kuona umuhimu wa kuhakikisha wanafunzi wote wanapata elimu stahiki na kutoa vitabu kwa wanafunzi wa darasa la nne kwa shule zote Mkoa wa Mwanza.
"Vitabu vilivyotolewa ni 6,482 kwa kila somo kwa masomo ya Hisabati,Kiinhereza,Kiswahili, Uraia na Maadili,Sayansi na Teknolojia na Maarifa ya Jamii hii inapelekea jumla ya vitabu 38,891,"alisema Mongella.
Kwa upande wake Afisa Elimu Msingi Ukerewe Mwl.Reginald Peter Richard akizungumzia hali ya elimu katika Wilaya hiyo amesema hali inaenda inabadirika kutoka walipokuwa kwani mwaka 2017 walifaulu kwa 52.7% lakini kwa mwaka 2018 kwa matokeo ya Mock yaliyotoka mwezi huu mwanzoni wamepanda kwa 61.5%.
"Malengo yetu ya Wilaya ni kufikia asilimia 80 na tumeishajipanga na tutafikia aailimia hizo kwani kwa kila shule sasa hivi tumeweka kambi kulingana na jografia kikata na kuunganisha shule 3
kama mikakati ya kuboresha na kuonfoa daraja "D" na "E" na kufaulu kwa A B C na lazma tutafikia huko,"alisema Mwl.Reginald.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Bw.Frank S.Bahati ameishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Rais wake Mhe. Dkt.John Magufuli kwa kuliana hili na kuwaletea vitabu ili kupunguza tatizo la upungufu wa vitabu katika Shule za Msingi.
"Sisi kama Wilaya tunaahidi kuvitunza vitabu hivi na kuvitumia kwa malengo tarajiwa ili kuinua kiwango cha ufaulu katika Wilaya yetu,"alisema Bahati.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.